PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE

PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE
kiungo : PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE

soma pia


PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ameiagiza Kampuni ya KGG Investment Ltd & Tanafri Group Ltd inayojenga Mradi wa Maji wa Mukabuye kuhakikisha inakamilisha mradi huo ifikapo mwezi Disemba, 2018 ili wakazi wa Mukabuye na vijiji jirani wapate huduma ya majisafi na salama. 

Profesa Mbarawa ametoa maagizo hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mukabuye kwenye ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma. “Mradi wa Maji wa Mukabuye umeanza kutekelezwa Juni, 2018 na unategemewa kukamilika mwezi Aprili, 2019 kulingana na mkataba. Lakini mimi nataka mkandarasi akamilishe mradi huu mwishoni mwa mwaka huu ili wananchi hawa wapate maji haraka iwezekanavyo’’, amesema Profesa Mbarawa. 

“Hakuna sababu ya kusubiri mpaka mwakani mradi huu ukamilike, kama fedha zipo na tutamlipa mkandarasi kiasi kilichobaki. Sina mashaka na uwezo wa mkandarasi kwa sababu uwezo anao, kikubwa ni kuongeza bidii na kasi ya utekelezaji’’, aliongeza Profesa Mbarawa. Akisisitiza ziara yake imelenga kubaini na kutatua changamoto zote za miradi ya maji katika Wilaya ya Kibondo kwa kuwa Serikali imelenga kuwa karibu na wananchi na kutatua kero zao kwa wakati. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Paul Bura (kushoto) mara baada ya ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Mukabuye, wilayani Kibondo katika Mkoa wa Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye kisima cha IOM kilichopo eneo la Kumwayi kinachotumiwa na Mradi wa Maji wa Kibondo Mjini, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Mabamba/Mukurazi uliopo Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akizungumza na viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo katika ofisi za wilaya, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akijibu maswali ya wakazi wa Kijiji cha Mukabuye kabla ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Mukabuye, wilayani Kibondo katika Mkoa wa Kigoma. 



Hivyo makala PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE

yaani makala yote PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/profesa-mbarawa-aweka-jiwe-la-msingi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE"

Post a Comment