DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE

DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE
kiungo : DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE

soma pia


DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kusimamia miradi ya maji kwa umakini mkubwa.

Amewataka DAWASA kuhakikisha kufikia 2020 asilimia 85 ya vijijini na asilimia 95 ya mijini inapata maji safi na salama. Mkumbo amesema hayo wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya jengo la Maji lililopo Ubungo jijini Dar es Salaama na linalotarajiwa kumalizaika Februari 2020.

Utiaji wa saini hiyo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. Akizungumza baada ya utiaji wa saini, Mkumbo amesema DAWASA lazima wahakikishe wanasimamia mapato ili kuweza kuendeleza miradi ya maji ili wananchi waweze kufaidika.

Amesema, hafla ya leo sio ya kukabidhiwa jengo tu ila wanatakiwa kusimamia mradi wa Kidunda, visima vya Kimbiji Mpera pamoja na kuwaunganishia wateja wapya. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi Mwamunyage amesema changamoto kubwa iliyokuwepo katika mamlaka hiyo ni maeneo ya kufanyia kazi ila baada ya kukabidhiwa jengo hilo wanaamini kwa sasa kazi zitafanyika kwa wakati.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa DAWASA kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa machache.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni kulia ni mmoja ya wajenzi wa kampuni ya CCECC ambao ndiyo wakandarasi. Wafanyakazi wa DAWASA na wageni waalikwa wakifuatiliwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage (anayefuata kushoto) wakifurahi pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) mara baada ya kuzindua picha ya jengo la Maji linalotarajiwa kumalizika Februari 2020.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE

yaani makala yote DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/dawasa-yatakiwa-kufanyakazi-kwa-bidii.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DAWASA YATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YAKE"

Post a Comment