title : SUMATRA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO
kiungo : SUMATRA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO
SUMATRA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO
Na EmanuelMadafa,Mbeya.
MAMLAKA ya Udhibiti na Usafirishaji wa Nchi Kavu na Reli, (SUMATRA),imeanza kutekeleza agizo la Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi . Atashasta Nditiye,ambalo lilielekeza kuanza kutoa elimu kwa wadau na watumiaji usafiri njia ya reli ili kupunguza vitendo vya uhujumu uchumi vinavyofanywa na watu ambao si waadilifu.
Akizungumza Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya Mdhibiti na Mkaguzi wa Usalama wa Reli, kutoka Mamlaka ya Udhibiti SUMATRA, Mhandisi . Hanya Mbawala,amesema tayari Mamlaka hiyo imenza kutekeleza agizo la Waziri ambapo wameanza kutoa elimu hiyo kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa reli hiyo katika stesheni ya Chimala.
Amesema, kazi ya kitengo cha reli ndani ya SUMATRA ni kuhakikisha usafiri wa reli unakua salama na uhakika na jambo hilo linafanyika kwa kitengo kuendesha kaguzi za mara kwa mara ikiwa na kuishauri serikali na TAZARA kwa ujumla ya nini kifanyike.
Amefafanua kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mwezi Mei mwaka huu akiwa Ifakara, alitoa maagizo ambayo tayari mamlaka imeanza kuyafanyia kazi, hivyo hatua iliyopo kwa sasa ni kutoa elimu kwa wadau na watumiaji wa reli kuanzia eneo la Makambako hadi Tunduma.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Ndugu Rubeni Mfune akizungumza na Viongozi wa vijiji na wananchi (hawapo pichani)ambao wana ishi maeneo ya jirani na njia ya Reli ya Tazara katika Stesheni ya Chimala Wilayani humo .
Mdhibiti na Mkaguzi wa Uslama wa Reli, kutoka Mamlaka ya Udhibiti SUMATRA, Eng. Hanya Mbawala akisisitiza jambo katika mkutano na wananchi na watendaji wa vijiji (hawapo pichani) ambao wanaishi pembezoni na njia ya reli ya Tazara katika stesheni ya Chimala wilayani Mbarali Mkoani Mbeya June 29 ,2018.
Meneja Usalama wa Reli ya Tazara Ndugu Sadick Anthony akizungumza na wananchi na Viongozi wa vijiji wanaoishi pembezoni mwa reli ya Tazara (hawapo pichani)katika mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Sumatra kwa lengo la kutoa elimu juu ya ulinzi wa reli ya Tazara .
Wananchi na Viongozi wanaoishi pembezoni mwa Reli ya Tazara katika Stesheni ya Chimala Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa katika mkutano uliotishwa na viongozi wa Sumatra na Tazara katika kutoa elimu ya ulinzi wa Reli hiyo.
Hivyo makala SUMATRA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO
yaani makala yote SUMATRA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SUMATRA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/sumatra-yaanza-kutekeleza-agizo-la.html
0 Response to "SUMATRA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO"
Post a Comment