title : MFANYABIASHARA APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTOA RUSHWA
kiungo : MFANYABIASHARA APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTOA RUSHWA
MFANYABIASHARA APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTOA RUSHWA
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imempandisha kizimbani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone, Mohamed Kiluwa (50) kwa tuhuma za kutoa rushwa Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.
Mshtakiwa huyo amepandiashwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 2, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi ambapo amesomewa shtaka moja la kujihusisha na vitendo ya rushwa.
Akisoma shtaka hilo, wakili wa Serikali Mkuu kutoka Takukuru, Maghela Ndimbo amedai Julai 16, 2018 mshtakiwa huyo akiwa kama Mkurugenzi wa kampuni hizo mbili alitoa rushwa ya USD 40,000 sawa na Sh. Milioni 90 kwa Waziri Lukuvi.
Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alitoa fedha hizo kwa lengo la kutowasilisha hati ya umiliki wa kiwanja namba 57 Block B Kikongo na D Disunyura kilichopo eneo la viwanda lililopo Kibaha mkoani Pwani.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana. Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho vinayotambulika.
Aidha mmoja kati yao ametakiwa kutoa Fedha taslimu Sh. Milioni 45 na kama hana awasilishe hati ya mali isiyo amishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Agosti 15, mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa.

Hivyo makala MFANYABIASHARA APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTOA RUSHWA
yaani makala yote MFANYABIASHARA APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTOA RUSHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MFANYABIASHARA APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTOA RUSHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mfanyabiashara-apandishwa-kizimbani-kwa.html
0 Response to "MFANYABIASHARA APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTOA RUSHWA"
Post a Comment