title : DKT. MWANJELWA ATAO WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO, KULIMA KILIMO CHENYE TIJA
kiungo : DKT. MWANJELWA ATAO WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO, KULIMA KILIMO CHENYE TIJA
DKT. MWANJELWA ATAO WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO, KULIMA KILIMO CHENYE TIJA
Na Stella Kalinga, Simiyu
Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mwanjelwa ametoa wito kwa wakulima kote nchini kulima kilimo chenye tija kwa kutumia zana bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji na kupata mavuno mengi na bora.
Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo Agosti Mosi, mara baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya Kilimo katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Bariadi, katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu.
Dkt. Mwanjelwa amesema Serikali kupitia Mfuko wa pembejeo unatoa mkopo wa pembejeo kwa riba ndogo sana, hivyo akatoa wito kwa wakulima wote nchini kwenda katika Halmashuri zao na kupata utaratibu wa kuomba mikopo hiyo ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kununua zana bora za kilimo.
“ Nitoe wito kwa wakulima wote nchini wajitahidi sana kwenda kwenye kulima kilimo cha kisasa kilimo chenye tija, sisi kama Serikali tuna mfuko wetu wa pembejeo unaotoa mikopo kwa riba ndogo sana, hivyo wakulima wanaweza kuomba mikopo hiyo na kwenda kununua pembejeo bora za Kilimo” alisema Dkt. Mwanjelwa.
Katika hatua nyingine Dkt. Mwanjelwa amewataka maafisa ugani kuwafuata wakulima shambani badala ya kukaa ofisini, ili kuwapa elimu ya kilimo bora na kuwawezesha wakulima kufikia lengo la kulima kilimo chenye tija.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa akikagua mashamba darasa ya JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi leo Agosti Mosi, 2018, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa akikagua mashamba darasa ya JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi leo Agosti Mosi, 2018, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Mtaalam wa kutoka Jeshi la Magereza akitoa maelezo kwa Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa wakati walipotembelea mabanda ya maonesho ya mifugo ya Jeshi hilo katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji Bariadi, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Mtaalam wa Ufugaji wa Samaki kutoka JKT, Luteni Joseph Lyakurwa(kulia) akitoa maelezo kwa Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa (wa tatu kushoto) na Omary Mgumba (kushoto) wakati walipotembelea mashamba darasa ya JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji Bariadi, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa Jeshi la Magereza akitoa maelezo ya namna ya kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya mimea kwa Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa (wa tatu kulia) na Omary Mgumba (wa pili kulia) wakati walipotembelea mabanda ya maonesho ya Jeshi hilo katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji Bariadi, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa akipewa maelezo kuhusu zana na mashine za kisasa na wataalam wa JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi leo Agosti Mosi, 2018, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DKT. MWANJELWA ATAO WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO, KULIMA KILIMO CHENYE TIJA
yaani makala yote DKT. MWANJELWA ATAO WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO, KULIMA KILIMO CHENYE TIJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT. MWANJELWA ATAO WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO, KULIMA KILIMO CHENYE TIJA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dkt-mwanjelwa-atao-wito-kwa-wakulima.html
0 Response to "DKT. MWANJELWA ATAO WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO, KULIMA KILIMO CHENYE TIJA"
Post a Comment