BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc

BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc
kiungo : BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc

soma pia


BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeridhia ombi la uunganishwaji wa benki za Benki ya Wanawake Tanzania(TWB) pamoja na TPB Bank Plc.

Kutokana na hatua hiyo sasa kutakuwa na benki moja kuanzia Agosti 3 mwaka huu itakayoendelea kuitwa benki ya TPB Bank Plc ambayo itaendelea kuwa na mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Florenc Luoga amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na ombi la wanahisa la kutaka kuunganishwa kwa benki hizo. Amesema hivyo kuanzia sasa wateja, wafanyakazi , mali a madeni yote ya TWB yataunganishwa na yale ya benki ya TPB huku akifafanua muunganiko wa benki hizo unaifanya benki ya mpya ya TPB Bank Plc kuwa imara zaidi na itakuwa ina mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa chini ya kifungu cha 17 cha sheria ya mabenki na taasisi za fedha.

"Benki Kuu inawaomba wateja wa benki ya TWB kuwa watulivu katika kipindi hiki cha mpito cha uunganishwaji wa benki hizi na watendelea kupata huduma za kibenki kwa utaratibu utakaotolewa na menejimenti ya uongozi wa benki ya TPB,"amesema Profesa Luoga. Wakati huo huo amesema Benki za TOBACO na KCBL kwa sasa zimeweza kuongeza mtaji na kukidhi kiwango kinachohitajika kisheria na hivyo zinaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Amesema BoT inawagakikisha wananchi kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha. Awali Gavana Luoga amefafanua Januari 4 mwaka huu BoT iliongeza muda wa miezi sita kwa benki tatu ambazo ni Tandahimba Community Bank Limited (TOBACO), Tanzania Women's Bank Plc(TWB) na Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL).

Ambapo mpaka Juni 30 mwaka huu ili kufikisha kiwango cha mtaji kinachohitajika na sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2007 na kanuni zake za kiwango cha chini cha mtaji cha Sh.bilioni mbili kwa benki za wananchi. Aidha benki hizo ziliongezewa muda wa mwezi mmoja hadi Julai 31 mwaka 2018 ili kukamilisha taratibu za kuongeza mtaji.

Kutokana na kutolewa kwa muda huo ndipo wanahisa wa TWB na TPB walipoamua kuunganisha benki hizo na BoT imeridhia.


Hivyo makala BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc

yaani makala yote BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/bot-yaridhia-uunganishwaji-wa-benki-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc"

Post a Comment