title : NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI
kiungo : NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi wanaozunguka hifadhi za misitu katika wilaya ya Kisarawe kuzingatia mipaka iliyowekwa pamoja na matumizi ya ardhi ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baina ya wananchi na serikali.
Hasunga alisema jana kwenye ziara aliyoifanya alipotembelea Kiwanda cha Caoline, pamoja na msitu wa hifadhi Kazimzumbwi na Pugu.Alisema serikali haitakubali kuona maeneo ya hifadhi yanavamiwa ovyo na wananchi ama mifugo kuachiliwa bila utaratibu maalum.
“Kuna umuhimu mkubwa wa kukuza sekta ya utalii. Wataalii wengi wanapenda kuona misitu. Hii ni sehemu ya utalii,” alisema.Aliwataka Kisarawe kuangalia vivutio walivyonavyo ili kuboresha katika maeneo hayo kwa ajili ya kuvutia utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kutoka makao makuu Dar es Salaam akiangalia vitalu vya miche ya miti wakati alipowatembelea wanakijiji wa Maguruwe wanaopakana na msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi waliojitolea kuotesha miche ya miti kwa ajili ya kupanda kwenye eneo la msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo ( wa kwanza kushoto) wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki ya kutembelea kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam wakioneshwa ramani ya Msitu wa Hifadhi Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo ( wa tatu kushoto) kuhusiana na“eneo la msitu huo lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-wa-maliasili-na-utalii_27.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI"
Post a Comment