title : HALMASHAURI 182 ZAKAIDI ZADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM
kiungo : HALMASHAURI 182 ZAKAIDI ZADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM
HALMASHAURI 182 ZAKAIDI ZADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
HALMASHAURI 182 nchini ikiwemo saba za mkoani Pwani ,zinadaiwa kutumia vibaya mabilioni ya fedha yaliyotumika kuondoa zaidi ya lita 100,000 za dawa ya viuadudu vya mazalia ya mbu ,zilizokosa soko katika kiwanda cha Biotech Products Limited,kilichopo Mji Wa Kibaha ,ikiwa ni agizo alilolitoa Rais Dkt.John Magufuli June 22 mwaka jana.
Aidha halmashauri ambazo zinadaiwa kiasi cha sh.bil.1.8 walizochukulia dawa hiyo zimetakiwa kulipa fedha hiyo haraka ili kiwanda kiweze kujiendesha na kulipa watumishi wake mishahara.
Akizungumza katika ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa ya viuadudu inayozalishwa katika kiwanda hicho ,meneja wa udhibiti wa ubora na viwango kiwandani hapo , Samwel Mziray , alisema ni halmashauri mbili pekee zilizochukua dawa hiyo kwa awamu ya pili.
Alieleza halmashauri 184 zilichukua dawa kwa awamu ya kwanza na ya pili zaidi ya lita 200,000 ambazo wameziweka stoo bila kuzitumia wakidai hawana fedha ya kununulia pampu."Wanashindwa kuzitumia kutokana na kukosa pampu ya kupulizia ,hii ni aibu ,nimesikitishwa sana na hali hii, "
"Ni ngumu na jambo la ajabu leo hii Rais atoke kuja kufuatilia agizo lake ama kuzifuatilia halmashauri hizo, serikali ina nia njema lakini watendaji tunashusha juhudi za Rais na serikali ""Ninawaomba wakuu wa mikoa mingine nchini kuiga mfano wa mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ya kuhamasisha kununua dawa hizo, ili kupambana na vita dhidi ya ugonjwa hatari wa malaria." alieleza Mziray .
Mziray alieleza baada ya agizo la Rais walianza na mikoa 14 katika halmashauri 96 na awamu ya pili waligawa kwenye halmashauri za mikoa 12 na kutimiza mikoa 26 na halmashauri 184 nchini .Hata hivyo baada ya mgao wa kwanza halmashauri ya Rufiji iliongeza Lita 540 na Kibaha Vijijini waliongeza lita 520 .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo (wa kulia) ,akimkabidhi dawa ya viuadudu vya mazalia ya mbu ,mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze ,Edes Lukoa wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa hiyo ,Mkoani Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Meneja wa udhibiti wa ubora na viwango katika kiwanda kinachozalisha dawa ya viuadudu cha Tanzania Biotech Products Ltd kilichopo Mjini Kibaha akionyesha wananchi kuwa dawa hiyo haina madhara, wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa hiyo,Mkoani Pwani .(picha na Mwamvua Mwinyi).
Hivyo makala HALMASHAURI 182 ZAKAIDI ZADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM
yaani makala yote HALMASHAURI 182 ZAKAIDI ZADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALMASHAURI 182 ZAKAIDI ZADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/halmashauri-182-zakaidi-zadaiwa-kukaidi.html
0 Response to "HALMASHAURI 182 ZAKAIDI ZADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM"
Post a Comment