MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU

MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU
kiungo : MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU

soma pia


MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU

Na Baltazar Mashaka, Mwanza

Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Bwiru la jijini Mwanza limemtunuku cheti Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Alhaji Sibtain Meghjee kwa kutambua huduma za jamii zinazotolewa na taasisi hiyo katika sekta za afya,elimu na maji bila kujali itikadi za dini wala kubagua.

Akizungumza kabla ya hafla hiyo Mchungaji Ephafra Zabron alisema taasisi ya TD & CF imefanya mambo mengi muhimu ya kusaidia jamii kwa kuhudumia watu wa dini na madhehebu mbalimbali bila ubaguzi katika masuala ya afya, elimu na maji lakini pia imejenga shule, nyumba za ibada (misikiti na makanisa) na kuchimba visima.

“Tusipotoshwe na watu kuwa watu wa dini ya Kiislamu wana mitizamo tofauti na wapo watu wanapotosha na kuleta lugha za kufarakanisha watu kuwa ukimwona Muislamu ni adui yako si kweli.Waislamu wanatuzidi mambo mengi na wanatimiza maandiko kwa vitendo ambapo kila Ijumaa wanatoa misaada kwa jamii ya wahitaji,” alisema Mchungaji Ephafra. 

Mchungaji huyo alieleza kuwa Kanisa la AICT Bwiru linatambua mchango mkubwa wa Sibtain Meghjee na taasisi yake kwa jamii kwani anafanya huduma aliyoifanya Yesu na kuwataka waumini wa kanisa hilo na wakazi wa eneo la Bwiru wajifunze kutokana na kazi zinazofanywa na The Desk & Chair.
Mwenyekiti wa The Desk &Chair Foundation (TD &CF) Sibtain Meghjee (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Mchungaji Philipo Majuja kutokana na kutambua mvhango wa taasisi hiyo wa kusaidia jamii.Hafla iliyofanyika kanisani hapo Jumalipili iliyopita.
Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Mchungaji Philipo Majuja (kushoto),akipokea kitabu cha Kuran tukufu kutoka kwa Mwenyekiti wa The Desk &Chair Foundation (TD &CF) Sibtain Meghjee. Anayeshuhudia kushoto wa kwanza ni Mchungaji wa Kanisa la Bwiru, Ephafra zabron na kulia ni Sheikh wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya ziwa Hashimu Ramadhan.Picha na Baltazar Mashaka



Hivyo makala MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU

yaani makala yote MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/meghjee-atunukiwa-cheti-na-kanisa-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU"

Post a Comment