title : MAKATIBU WAKUU WAJADILI UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE
kiungo : MAKATIBU WAKUU WAJADILI UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE
MAKATIBU WAKUU WAJADILI UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE
Na Veronica Simba
Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, hivi karibuni walifanya kikao kujadili hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa kufua umeme kutoka katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge.
Kikao hicho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
Aidha, kikao hicho pia kilijadili majukumu ya kila Wizara husika katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi huo.
Akifungua kikao hicho, Dkt. Mwinyimvua alieleza kuwa mahitaji ya umeme nchini kwa sasa ni makubwa kutokana na kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda hali inayosababisha huduma ya umeme wa uhakika kuhitajika zaidi ya muda mwingine wowote.
“Serikali ya Awamu ya Tano inaelekeza nchi kuingia kwenye uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025. Ili kufikia malengo hayo, hatua za makusudi za kuongeza uzalishaji wa umeme kwa ajili ya viwanda zinahitajika.”
Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, akielezea umuhimu wa Mradi huo kwa Taifa alisema kuwa umeme wa uhakika unahitajika ili pamoja na mambo mengine kukidhi mahitaji ya mkakati wa kusambaza umeme vijijini ambao unaendelea nchini kote.
Awali, akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Mradi husika katika kikao hicho, Msimamizi wake, Mhandisi Leonard Masanja alieleza kuwa, Desemba 19 mwaka huu, Wizara ya Nishati ilitangaza zabuni ya kumpata Mkandarasi wa Ujenzi wa Mradi huo ambao utekelezaji wake unakadiriwa kuanza mwishoni mwa mwezi Februari 2018.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali (hawapo pichani) kujadili Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge, hivi karibuni mjini Dodoma.
Msimamizi wa Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge, Mhandisi Leonard Masanja, akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Mradi huo, wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali (hawapo pichani), kilichofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
Ramani ya Mradi wa kufua umeme kutoka katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge, utakavyoonekana baada ya kukamilika.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAKATIBU WAKUU WAJADILI UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE
yaani makala yote MAKATIBU WAKUU WAJADILI UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKATIBU WAKUU WAJADILI UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/makatibu-wakuu-wajadili-utekelezaji.html
0 Response to "MAKATIBU WAKUU WAJADILI UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE"
Post a Comment