title : MILIONI 250/- KUTUMIKA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WALIOTELEKEZWA DAR
kiungo : MILIONI 250/- KUTUMIKA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WALIOTELEKEZWA DAR
MILIONI 250/- KUTUMIKA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WALIOTELEKEZWA DAR
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na jukumu la kuwasaidia wanawake ambao wamezalishwa watoto na kisha kutelekezwa na waume zao huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Sh.milioni 250 ndizo zitakazotumika katika kuwakatia bima ya afya watoto zaidi ya 1500 waliotelekezwa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mbele ya umati mkubwa wa akina mama ambao wamefika ofisini kwake kupata msaada huo baada ya kuutangaza kuwasaidia wanawake wa mkoa wake ambao wametelekezwa, amesema anashukuru wadau mbalimbali wameendelea kujitokza na kusaidia watoto hao.
Amefafanua kuwa katika suala la bima ya afya kwa watoto hao ni kwamba jumla ya Sh.milioni 250 zinatarajia kutumika kwa ajili ya kuwakatia bima hiyo ya afya ambayo itawezesha kupata tiba.
"Kuna mdau mmoja kutoka Afrika Kusini ameahidi kuwasaidia watoto hao katika suala la afya hasa katika kupata bima ya afya na tayari mchakato huo umeanza leo hii na mdau huyo ameahidi kusaidia watoto zaidi ya 1500 ambao watagharimu kiasi hicho cha fedha,"amesema Makonda.
Kuhusu sifa za watoto watakaopatiwa bima za afya bure ambayo ni ya mwaka mmoja,Makonda amesema lazima mtoto awe ametelekezwa, awe raia wa Tanzania na awe na umri usiozidi miaka 18.
Kwa upande wa Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Wilaya ya Kinondoni Magreth Malangila ameeleza ili kukamilisha mchakato huo wazazi waje na picha (pasport) ya rangi ya bluu na cheti cha kuzaliwa.
Hivyo makala MILIONI 250/- KUTUMIKA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WALIOTELEKEZWA DAR
yaani makala yote MILIONI 250/- KUTUMIKA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WALIOTELEKEZWA DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MILIONI 250/- KUTUMIKA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WALIOTELEKEZWA DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/milioni-250-kutumika-kuwakatia-bima-ya.html
0 Response to "MILIONI 250/- KUTUMIKA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WALIOTELEKEZWA DAR"
Post a Comment