title : TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO
kiungo : TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO
TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO
Na Fatma Salum – MAELEZO.
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imeendelea kuiasa jamii kuhusu kubadili tabia ili kuepuka maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani ugonjwa huo bado ni janga kwenye nchi yetu.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo Bw.Jumanne Issango alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio na changamoto za tume tangu ilipoanza kutekeleza majukumu yake.
“UKIMWI bado ni changamoto katika maendeleo ya Taifa letu na umeendelea kuathiri kila sekta, kila imani, matajiri na masikini nchini kote hivyo ni wajibu wa kila mmoja kujitathmini mwenendo wake na kuacha tabia hatarishi ambazo zinachangia kuongeza maambukizi ikiwemo uasherati, ngono zembe, ulevi na kadhalika,” alisema Issango.
Alieleza kuwa kwa miaka ya karibuni hali ya maambukizi ya UKIMWI imeendelea kupungua ingawa kuna tofauti kwenye mikoa, wilaya na makundi ya kijamii.Issango alibainisha kuwa kiwango cha maambukizi Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na takwimu hizo ni kutokana na Utafiti wa Viashiria vya UKIMWI mwaka 2012.

Kaimu Mkrugenzi Mkuu wa TACAIDS Bw.Jumanne Issango akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano kuhusu changamoto na mafanikio katika kupambana na virusi vya ukimwi nchini kulia ni Kaimu Mkurugenzi Muitiko wa kitaifa wa TACAIDS Bi.Audrey Njelekela mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za TACAIDS leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
Hivyo makala TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO
yaani makala yote TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/tacaids-ukimwi-bado-ni-changamoto.html
0 Response to "TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO"
Post a Comment