title : SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA
kiungo : SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA
SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA
CHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama wilayani Longido mkoani Arusha kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 15.8.
Waziri Mkuu ameweka jiwe hilo la msingi leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Longido Mjini pamoja na kijiji cha Oltepesi ambao chanzo chake ni kutoka mto Simba wilaya ya Hai mkoani Kilimanajro.
Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kupeleta wataalamu wilayani Longido ambao watashirikiana na Halmashuri za wilaya ya Longido na tarafa ya Loliondo kutafuta vyanzo vingine vya maji ili wananchi waweze kupata maji ya kutosha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye eneo la uwekaji jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arusha, Septemba 21, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Longido kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha Septemba 21, 2017.
Baadhi ya Wananchi wa Longido wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa wakati alipozungumza kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha, Septemba 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA
yaani makala yote SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/shida-ya-maji-longido-kuwa-historia.html
0 Response to "SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA"
Post a Comment