title : DONGE NONO KUTOLEWA KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MITA ZA MAJI JIJINI MWANZA
kiungo : DONGE NONO KUTOLEWA KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MITA ZA MAJI JIJINI MWANZA
DONGE NONO KUTOLEWA KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MITA ZA MAJI JIJINI MWANZA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) imesema itatoa zawadi nono kwa wananchi watakaofanikisha kukamatwa kwa wezi wa mita za maji jijiini humo. Akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Mwanza hapo jana, Meneja Msaidizi- Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Mohamed Saif alibainisha kwamba kumekuwepo na wimbi la wizi wa mita za maji kwenye maeneo mbalimbalii jijini humo.
Saif alisema jitihada mbalimbali zinaendelea kuwasaka wanaojihusisha na matukio hayo ya wizi na alibainisha kwamba mwananchi atakayefanikisha kuwabaini na kuwafichua wezi hao atapewa zawadi nono. Hata hivyo, Saif hakuweka bayana zawadi itakayotolewa lakini alimthibitishia mwandishi wa habari hii kwamba Mamlaka imeandaa zawadi nono ambayo mtoaji wa taarifa itakayofanikisha kuwakamata wezi hao ataifurahia.
“Ninawathibitishia kwamba mwananchi atakayefanikisha kuwafichua hawa wanaojihusisha na matukio haya ya wizi. Mamlaka itamzawadia zawadi nzuri ambayo naamini ataifurahia,” alisema.
Alilaani matukio hayo ambayo yanaendelea kushamiri kwenye maeneo mbalimbali Jijini humo ambayo alisema yanaipotezea mapato makubwa Serikali na pia yanasababisha upotevu mkubwa wa maji kwenye maeneo husika.
"Wahujumu hao huwa wanafungua mita za maji na kuziiba huku nyuma wakiacha mabomba yanamwaga maji mengi ambayo kimsingi yanapotea na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa maji suala ambalo linaisababishia hasara kubwa Serikali," alisema.
Saif alisema ndani ya kipindi cha Mwezi mmoja kuanzia Agosti hadi Septemba mwaka huu, idadi ya mita za maji zilizoibiwa jijini humo imefikia mita 170. Aliongeza kuwa upotevu wa maji unaotokana na wizi wa mita unasababisha kuzorota kwa huduma ya usambazaji majisafi kwani gharama inayopaswa kutumika mahali pengine ikiwemo uboreshaji wa huduma na pia kuunganishia wateja wapya inatumika kwenye ununuzi na ukarabati wa miundombinu hiyo iliyoibiwa au iliyoharibiwa wakati wa matukio hayo ya wizi.
Aidha, alisema MWAUWASA kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama imejipanga kuhakikisha hujuma hizo zinakomeshwa na aliwaasa wananchi kutoa ushirikiano katika hilo na pia aliziomba Serikali za Mitaa kuimarisha ulinzi shirikishi katika mitaa yao kwa lengo la kudhibiti wimbi la wizi wa mita za maji kwenye maeneo yao.
Hivyo makala DONGE NONO KUTOLEWA KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MITA ZA MAJI JIJINI MWANZA
yaani makala yote DONGE NONO KUTOLEWA KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MITA ZA MAJI JIJINI MWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DONGE NONO KUTOLEWA KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MITA ZA MAJI JIJINI MWANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/donge-nono-kutolewa-kwa-watakaofichua.html
0 Response to "DONGE NONO KUTOLEWA KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MITA ZA MAJI JIJINI MWANZA"
Post a Comment