Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko

Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko
kiungo : Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko

soma pia


Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko

MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, jana amekabidhiwa fedha zake alizoshinda kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko, jumla ya Sh Milioni 20.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana mkoani Mtwara katika benki ya NMB, ambapo Lukinga aliishukuru Biko na kusema kuwa fedha hizo atazitumia vizuri kuhakikisha zinakuza uchumi wake.“Nashukuru kwa kukabidhiwa fedha hizi ambazo kwa hakika nitazitumia vizuri kama sehemu ya kupiga hatua kiuchumi kama dhamira ya Biko kuanzisha bahati nasibu yao.

“Awali sikuamini kama naweza kushinda donge nono la Sh Milioni 20, hivyo ni wakati huu Watanzania wote kuamini kwamba Biko ni mchezo wa kubahatisha wa watu wote, maana kama hata mimi wa Mtwara nashinda, ndio kusema yoyote anaweza kushinda,” Alisema.


Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles, alimpongeza Lukinga kwa kukabidhiwa fedha zake, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa ya Biko ili washinde zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kila wakati, sambamba na droo kubwa ya Sh Milioni 20 inayotoka Jumatano na Jumapili.


“Jumapili hii amepata Lukinga ambapo leo tumemkabidhi fedha zake, hivyo wote mnaweza kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ya kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea kikiwa Sh 1,000 na kuendelea,” Alisema.


Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven mwenye fulana ya Biko kushoto akiwa ameshika hundi saa chache kabla ya kumkabidhi kiasi cha fedha cha Sh Milioni 20 mshindi wa Mtwara, Ally Hassan Lukinga katikati. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.


Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko Tanzania, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia, akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa mjini Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyeshinda katika droo ya 24 Jumapili. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko

yaani makala yote Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/mfanyakazi-wa-tanesco-mtwara-akabidhiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko"

Post a Comment