BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI

BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI
kiungo : BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI

soma pia


BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa seti za Jezi Mwenyekiti wa Timu ya Soka ya Muembe Ladu Omar Zubeir katika lengo la kuendeleza Michezo Nchini,Wa kwanza kutoka Kushoto ni Kocha wa Timu ya Soka ya Muembe Ladu Ramadhan Madundo na wa kwanza kutoka Kulia ni Katibu wa Timu hiyo Mohamed Mbarouk.
Mwenyekiti wa Timu ya Soka ya Muembe Ladu Omar Zubeir akimshukuru Balozi Seif kwa msaada huo wa Jeziutakaoleta faraja kwa Uongozi wa Klabu hiyo pamoja na Wachezaji wenyewe.


Balozi Seif Ali Iddi akisisitiza umuhimu wa kudumishwa nidhamu Michezoni ili wachezaji wajijengee heshima itakayowatanulia hatma njema kimichezo ikiwemo suala la ajira mara baada ya kukabidhi msaada wa Jezi.Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema suala la nidhamu michezoni ni jambo la msingi linalomjengea sifa na mafanikio mazuri mchezaji katika maisha yake Kimichezo.

Amesema mchezaji anapofikia hatua ya kutegemewa na Viongozi pamoja na walimu wake kutokana na kipaji alichojaaliwa analazimika kulinda heshima hiyo ili imfikishe daraja analokusudia kufikia hasa suala la ajira.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akiukabidhi Msaada wa seti mbili za Jezi pamoja naahadi ya Mipira Minne kwa Timu ya Soka ya Muembe Ladu katika azma ya kuunga mkono jitihada za kuendeleza Sekta ya Michezo Nchini.

Alisema nidhamu ndio silaha pekee inayomfikisha kwenye mafanikio Mchezaji au mtu yoyote katika malengo yake akatolea mfano baadhi ya Wachezaji wa Tanzania ambao kwa sasa wanacheza mpira wa kilipwa katika Timu za Mataifa mbali mbali Duniani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Timu ya Soka ya Muembe Ladu kwa jitihada unazochukuwa wa kuwaendeleza Vijana wao Kimichezo na kuweka Historia ya Timu hiyo katika medani ya Soka.

Akipokea Msaada huo Mwenyekiti wa Klabu ya Soka ya Muembe Ladu Omar Zubeir alimshukuru Balozi Seif kwa uamuzi wake wa kuisaidia Klabu hiyo msaada utakaoleta faraja kwao na hata wachezaji wenyewe.

Omar Zubeir alisema Timu ya Soka ya Muembe Ladu na Ujamaa zina Historia ndefu ya kuwa Timu Moja kipindi cha nyuma isiyosahaulika kwa wapenda soka Nchini kitendo ambacho Kizazi cha sasa kinapaswa kuifuatilia Historia hiyo.

Othman Khamis Ame & Rashida Abdi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.


Hivyo makala BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI

yaani makala yote BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/balozi-seif-ahimiza-nidhamu-michezoni.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BALOZI SEIF AHIMIZA NIDHAMU MICHEZONI"

Post a Comment