title : AU WAANDAA MKAKATI WA SOKO HURU LA BIDHAA KWA NCHI ZA BARA HILO
kiungo : AU WAANDAA MKAKATI WA SOKO HURU LA BIDHAA KWA NCHI ZA BARA HILO
AU WAANDAA MKAKATI WA SOKO HURU LA BIDHAA KWA NCHI ZA BARA HILO
Jumuiya ya Afrika (AU) ipo katika mkakati wa kukamilisha uwepo wa soko huru la bidhaa ambapo Kwa sasa ipo kwenye mchakato wa baadhi ya bidhaa kufunguliwa Kwa zaidi ya asilimia 90 ambapo Tanzania inatarajiwa kunufaika katika soko hilo.
Akizungumza katika kongamano lililowakutanisha wataalamu wa biashara kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika mwakilishi wa wizara ya viwanda na biashara Thomas Mcharo alisema kuwa nchi hizo wanachama wataweza kuchagua bidhaa ambazo zitaweza kufunguliwa baada ya mkataba kuanza kufanyakazi ambapo Tanzania ipo njiani kuridhia mkataba huo.
Alisema kuwa uwepo wa Tanzania katika kongamano hilo ni kuona na kuufahamu zaidi mtangamano huo hivyo wakati wowote kuweza kuingia ikiwa ni faida ya nchi kwani Sera ya viwanda inaendana na masoko ya bidhaa tutakazozalisha hapa nchini
"Unajua Sera ya serikali ya awamu ya Tano ni uchumi wa Kati wa viwanda na kongamano hili tunajadili mkataba wa kubadilishana biadha katika nchi za Afrika utaona faida Kwa nchi katika kukuza biashara za bidhaa zetu"
Kwa upande wake mwakilishi wa mwenyekiti wa meza ya majadiliano ya biashara kutoka umoja wa nchi za Afrika Alexander Rubanga alisema kuwa kuondoa tozo hizo zotasaidia kukuwa Kwa biashara katika mataifa ya Afrika.
Aliziomba nchi ambazo hazijaridhia mkataba huo kuona umuhimu wa kuwepo makubaliano kuhusu soko la pamoja la bidhaa litakalosaidi bara la Afrika kukua kiuchumi.
Awali mtaalamu wa majadiliano kutoka time ya umoja wa Afrika Dkt.Halima Noor Abdi alisema kuwa mpaka sasa ni nchi 52 zimekwisha weka sahihi ambapo nchi zingine bado zinaendelea na majadiliano kuhusiana na umoja huo.
Amesema kuwa faida kubwa ya kujiunga na mkataba huo wa mtangamano utaidia nchi moja kuweza kuzalisha bidhaa ambazo zitaweza kuuzwa kwenye nchi nyingine barani humo.
Hivyo makala AU WAANDAA MKAKATI WA SOKO HURU LA BIDHAA KWA NCHI ZA BARA HILO
yaani makala yote AU WAANDAA MKAKATI WA SOKO HURU LA BIDHAA KWA NCHI ZA BARA HILO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AU WAANDAA MKAKATI WA SOKO HURU LA BIDHAA KWA NCHI ZA BARA HILO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/au-waandaa-mkakati-wa-soko-huru-la.html
0 Response to "AU WAANDAA MKAKATI WA SOKO HURU LA BIDHAA KWA NCHI ZA BARA HILO"
Post a Comment