title : KISANGA AWATAKA WAKAZI WA OYSTERBAY KUWA WALINZI KWENYE MAENEO YAO
kiungo : KISANGA AWATAKA WAKAZI WA OYSTERBAY KUWA WALINZI KWENYE MAENEO YAO
KISANGA AWATAKA WAKAZI WA OYSTERBAY KUWA WALINZI KWENYE MAENEO YAO
Na Khadija Seif,Globu ya jamii
MWENYEKITI Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) katika Tawi la Oysterbay Dar es Salaam Donald Kisanga ameendesha uchaguzi wa chipukizi huku akiwaomba wazazi kuruhusu watoto kushirikia kikamilifua.
Amesema chipukizi wanafundishwa mambo mbalimbali yenye maslahi kwa nchi yao yakiwamo ya uzalendo,uadilifu,kuwa imara na ukakamavu katika kulijenga ,kulitetea na kupigania kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.
Kisanga amesema hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo pia amepongeza juhudi na mikakati inayofanywa na Serikali chini ya Rais Dk.John Magufuli katika kuwatumikia Watanzania.
Pia Kisanga ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kutunza na kulinda mazingira na kutoa taarifa pindi wanapoona wahalifu wanaingia kwenye makazi kwani vitendo hivyo lazima vikomeshwe ili kuwepo na amani
Kisanga pia amezungumzia jitihada zinazofanywa na Serikali ya CCM katika kutoa mikopo ambapo imeweza kutoa mikopo kwa wananchi ambao wanatakiwa kuunda kikundi cha watu wa tano na kuwasilisha barua zenye maelezo kwa mjumbe wa nyumba 10.
Amezungumzia pia namna ambavyo vijana wengi wamekua wakijuhusisha na uhalifu katika fukwe za Coco Beach ambapo watu wengi hufanyiwa vitendo vibaya na wengine kusababisha kupoteza maisha .
Kisanga ameeleza namna ambavyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alivyotembelea eneo hilo la fukwe hizo wakati wa Siku ya Maadhimisho ya Mashujaa nchini.
Ambapo alishirikiana na wananchi kufanya usafi na kutoa tamko kwa Serikali kuboresha mazingira hayo ili kuwa kivutio kizuri zaidi kwa watu ambao wanafika maeneo hayo kwa ajili ya kudarizi.
Hivyo makala KISANGA AWATAKA WAKAZI WA OYSTERBAY KUWA WALINZI KWENYE MAENEO YAO
yaani makala yote KISANGA AWATAKA WAKAZI WA OYSTERBAY KUWA WALINZI KWENYE MAENEO YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KISANGA AWATAKA WAKAZI WA OYSTERBAY KUWA WALINZI KWENYE MAENEO YAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/kisanga-awataka-wakazi-wa-oysterbay.html
0 Response to "KISANGA AWATAKA WAKAZI WA OYSTERBAY KUWA WALINZI KWENYE MAENEO YAO"
Post a Comment