WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA.

WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA.
kiungo : WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA.

soma pia


WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA.


Na. John Luhende 
Mwambawahabari 
Wizara  ya Viwanda na Biashara,  imesema kuanzia mwaka 2015 hadi  sasa, kuna viwanda vipya zaidi ya 3,000 ambavyo wawekezaji wake ni kutoka nje ya nchi vinaendelea na uzalishaji.

Aidha, kati ya viwanda 176 vilivyobinafsishwa  14  vimechukuliwa na serikali kwa ajili ya kutafuta wawekezaji baada wa waliokuwa awali kushindwa kufikia malengo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda alisema kuwa katika viwanda hivyo vilivyobinafsishwa 88 vinafanya vizuri huku 76 vikiwa na changamoto ya malighafi.

Kakunda alisema kuwa viwanda 40 vilifungwa na Msajili wa Hazina alitoa notisi kwa kila kiwanda kuleta mpango kazi wa namna ya kufufua viwanda hivyo.

"Viwanda 26 vipo katika hatua mbalimbali hivyo tunaamini kuwa mpaka Juni tutafikia hatua nzuri kwa viwanda tulivyovichukua na tunaamini tutavifufua viwanda vyote ili tuweze kutoa ajira kwa watanzania," alisema Kakunda.

Alieleza kuwa wanahitaji kuongeza kasi kwenye viwanda vya ndani vitakavyoongeza uzalishaji kwa kutumia brand ya Tanzania.

"Katika ripoti ya Benki ya Dunia iliyotolewa mwaka jana inaonesha kuwa Tanzania inaongoza upande wa  kusafirisha mizigo kwa soko la SADC kutoka mtaji wa Dola za Marekani 397 hadi 4

Aliongeza " tunaongoza kwa usafirishaji wa ngano, sabuni, bidhaa za chuma, unga na saruji."
Alisisitiza kutokana na ripoti hiyo wanalenga kufanya vizuri  kwenye soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Aidha, serikali imeiahidi serikali ya Uingereza kwamba itaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kuendeleza mitaji yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cook.

Kakunda alisema wafanyabiashara kutoka Uingereza wanaajiri zaidi ya watanzania 30,000 hivyo wataendelea kushirikiana ili kuendeleza mitaji yao.

"Tumekubaliana kuboresha mazingira ya kufanyia biashara na kwamba kuanzia mwaka ujao wa fedha tutaanza kutekeleza programu ya Blue Print," alisema Kakunda.

Alifafanua kuwa balozi huyo aliyeambatana na ujumbe wake, waliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu, afya, maji na viwanda.


Hivyo makala WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA.

yaani makala yote WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/waziri-kakunda-serikali-itaendelea.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI KAKUNDA: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA ILI KULINDA MITAJI YA WAFANYABIASHARA."

Post a Comment