NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI

NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI
kiungo : NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI

soma pia


NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI

NA LUSUNGU HELELA- SONGWE
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga  ameanza ziara ya  kimkakati ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wanafunzi wa  shule za sekondari nchini lengo likiwa ni  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao kwa wanafunzi hao. 
Mhe. Hasunga amesema sekta ya utalii inaweza kuongeza pato lake maradufu iwapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  wataanza kujua umuhimu juu ya utalii wa ndani bado angali wakiwa wadogo.
Katika ziara hiyo aliyoianza mkoani Songwe wilayani Mbozi, Naibu Waziri Mhe. Hasunga ameweza kutembelea shule za Sekondari tatu ikiwemo Shule ya Kilimampimbi, Vwawa pamoja na  Ilolo ambapo amezungumza na wanafunzi pamoja na walimu   kuhusu umuhimu wa utalii wa ndani.
Amefafanua kuwa Wanafunzi ni mabalozi wakubwa wa mabadiliko, wanapopata elimu juu ya  utalii wa ndani wataweza kuifikisha kwa wazazi, walezi pamoja na jamii kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Mhe. Hasunga  ametoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliokuwa wakijibu maswali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Amesema sekta ya utalii inachangia  asilimia 17.5 ya pato la taifa na inaweza ikawa asilimia 30 kama kutajengeka utamaduni kwa jamii  wakiwa bado  wanafunzi   kuhusu umuhimu wa kutenga muda pamoja na pesa kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
‘’Nchi yetu imejaliwa kuwa na vivutio vingi lakini imekuwa haifanyi vizuri ukilinganisha na nchi kama Misri aambao wao hawana vivutio vingi kama tulivyonavyo sisi, Wenzetu wana magofu pekee lakini wametuacha mbali’’ amesema Mhe. Hasunga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kilimampimbi iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini  kwa lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao. 
 Baadhi ya wanafunzi wa Vwawa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Vwawa iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa  lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (katikati)  akizungumza na walimu wa  shule ya sekondari ya Vwawa  iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe mara baada ya kumaliza   kuzungumza na  wanafunzi wa shuke hiyo  kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilolo  iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa  lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi, Bi. Hossana Mshule wakati w akielekea kukagua baadhi ya majengo yaliyojengwa kwa mfuko wa jimbo la Vwawa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI

yaani makala yote NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/naibu-waziri-hasunga-ahamasisha-utalii.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI"

Post a Comment