title : TANGAZO LA KIFO CHA CLEMENT THOMAS NDELEOKASI SHAYO
kiungo : TANGAZO LA KIFO CHA CLEMENT THOMAS NDELEOKASI SHAYO
TANGAZO LA KIFO CHA CLEMENT THOMAS NDELEOKASI SHAYO
Selina Mushi wa Mlandizi Njia Panda JKT anasikitika kutangaza kifo cha mume wake mpendwa Clement Thomas Ndeleokasi Shayo kilichotokea Alhamsi tarehe 29, Novemba 2018 katika hospitali ya Muhimbili - Mloganzila.
Mazishi yalifanyika nyumbani kwa marehemu, Uparo-Kirua Vunjo Moshi, Kilimanjaro siku ya Jumanne tarehe 4 Desemba, 2018. Watoto wa marehemu, Frederick Clement Shayo na Regina Clement Shayo, pamoja na mama yao Selina Mushi na dada wa marehemu Clementina Thomas Shayo wakishirkiana na famlia ya Mtika na ukoo wote wa Shayo, pamoja na familia ya Lesiaki Mushi wanatoa shukrani za dhati kwa wauguzi wa hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kwa juhudi zao za kujaribu kuokoa maisha ya mpendwa wao Clement.
Shukrani zao za pekee zinatolewa kwa Sista Agatha wa kituo cha Afya cha Mtakatifu Joseph, Luguruni Dar es Salaam, ndugu, jamaa na marafiki wote waliomhudumia Clement wakati wa kuugua kwake. Marehemu aliugua akalazwa hospitali kwa muda mfupi na kuruhusiwa; kisha akapata stroke.
Kifo cha Clement kimekuwa mshtuko mkubwa kwa ndugu, jamaa, marafiki, na wote waliomfahamu Tanzania, Marekani na Canada. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe. Mwenyezi Mungu aipokee roho ya marehemu Clement katika Furaha ya Milele, Amina
Hivyo makala TANGAZO LA KIFO CHA CLEMENT THOMAS NDELEOKASI SHAYO
yaani makala yote TANGAZO LA KIFO CHA CLEMENT THOMAS NDELEOKASI SHAYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANGAZO LA KIFO CHA CLEMENT THOMAS NDELEOKASI SHAYO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/tangazo-la-kifo-cha-clement-thomas.html
0 Response to "TANGAZO LA KIFO CHA CLEMENT THOMAS NDELEOKASI SHAYO"
Post a Comment