DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA.

DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA.
kiungo : DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA.

soma pia


DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi –Taifa ameendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera Januari Mosi, 2019 kwa kutembelea Kiwanda cha Kusindika Kahawa cha TANICA kilichopo Bukoba Manispaa, Mkoani kagera na kuagiza Uongozi wa Kiwanda hicho kutafuta Masoko ya Kimataifa ikiwemo Nchi za nje kama vile China.

Akiwa katika Kiwanda cha TANICA Katibu Mkuu Dkt. Bashiru amekutana na kuzungumza na Bodi ya Usimamizi wa Kiwanda hicho na kuwataka Wasimamizi hao kuendesha kiwanda hicho katika mfumo wa Kitaasisi ya kibiashara inayojulikana Kimataifa, na kisasa zaidi, ili kuleta tija katika kile alichotaja kuwa ni Vita ya Kiuchumi, huku akishangazwa na Kahawa ya Kagera kushindwa kuuzika katika soko la Kimataifa kama China, wakati Uganda tayari wameweza kupenyeza hadi katika Soko hilo.

Aidha Dkt. Bashiru amefafanua kuwa Vita ya kiuchumi i wa Kitaifa na Uchumi wa kisasa ni ile hasa inayolenga kukidhi mahitaji ya Taifa kwanza, walengwa wakiwa ni Watanzania wenyewe kujikwamua Kiuchumi kutokana na fursa zinazowazunguka, huku akiagiza Uongozi wa Kiwanda hicho kuboresha miundo mbinu ya Kitekenelojia na kubuni miradi mingine zaidi kama Uvuvi, Mvinyo, Kusindika Ndizi n.k

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa TANICA Bwn. Linus R . Leopord Licha ya kubainisha baadhi ya mafanikio waliyoyapata kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Mei mpaka Oktoba Mwaka jana, ambayo ni pamoja Kuendelea kulipa madeni sugu ya Kiwanda hicho, wamefanikiwa pia kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni Nne,na huku wakiwa wameshachangia pato la Taifa zaidi ya shilingi Milioni Mia Nane, hakusita pia kuzitaja changamoto za Kiwanda hicho, ambazo ni pamoja na Uongozi uliopo madarakani kutishiwa Vifo na waliokuwa wafanyakazi na Viongozi walioachishwa Kazi, Kugushiwa kwa Nembo ya Kampuni na kusababisha Kuchafuliwa kwa Soko la Kahawa yao, Hali ya Mishahara na Ajira kwa wafanyakazi wenye Taaluma.

Awali Dkt. Bashiru amepata fursa ya kutembelea Bandari Ndogo ya Kemondo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na kuzungumza na Wananchi wa maeneo yale pamoja na Viongozi wa Serikali na Kichama. Miongoni mwa maelekezo aliyoyatoa ni juu ya Uongozi wa Bandari hiyo kuangalia upya namna ya Tozo inayolipwa getini kwa sasa, pia Tozo inayolipwa kwa Kampuni inayojihusha na Ubebaji mizigo, sambamba na Uvuvi haramu na kuutaka Uongozi husika kubainisha wahusika wa vitendo hivyo ili watiwe Nguvuni na sheria ichukue mkondo wake.
Dkt. Bashiru Kakurwa Akipata maelezo ya Bidhaa ya Kahawa kutoka kwa Rewina Peter (Afsa masoko - TANICA) mara baada ya kuwasili Kiwandani hapo.
Meneja Mkuu wa TANICA Bwn. Linus R. Leopord akitoa ufafanuzi Kwa Dkt. Bashiru namna ya kupeleka Bidhaa yao katika Soko la Kimataifa.
Pichani dkt. Bashiru akizungumza na wannchi katika Bandari ya Kemondo, pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Bwn. Murshidi Ngeze.
Wajumbe wa Bodi ya TANICA pamoja na Uongozi wakiwa wameketi Kikao na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru.


Hivyo makala DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA.

yaani makala yote DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/dkt-bashiru-wawekezaji-wa-kiuchumi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA."

Post a Comment