WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI

WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI
kiungo : WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI

soma pia


WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Taasisi ya Tiba Mifupa (MOI), Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani wameendesha kambi maalum ya kutoa huduma za kibingwa kupitia tiba Radiolojia ambapo wagonjwa 23 wamenufaika na tiba hiyo.

Tiba hiyo inahusisha utaalam wa kutumia vifaa vya Radiolojia kama X-Ray, MRI, CT-Scan na Ultra- Sound kutibu moja kwa moja ugonjwa au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Radiolojia MNH, Dkt. Flora Lwakatare amesema huduma hiyo ya kibingwa ilianza kwa mara ya kwanza nchini Novemba mwaka jana ambapo kabla ya uanzishwaji wake wagonjwa waliokuwa wanahitaji huduma hizi walikuwa wakienda nje ya nchi.

Akielezea kuhusu huduma zilizitolewa katika kambi hiyo amesema ni utoaji wa sampuli kutoka kwenye vivimbe katika sehemu mbalimbali za mwili ambazo si rahisi kufikiwa bila upasuaji mkubwa, kuzibua mirija ya nyongo, kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya mkojo imeziba na unyonyaji wa vivimbe vyenye maji au usaha.‘‘Kambi hii imehusisha wakufunzi ambao ni madaktari bingwa, mafundi sanifu Radiolojia, wauguzi Radiolojia kutoka vyuo vikuu vya Yale na Emory. Pia, watalaam kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa na CCBRT nao wananufaika na mafunzo hayo.’’
Mkuu wa Idara ya Radiolojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Flora Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari juu ya wataalam kuzibua njia ya nyongo ya mgonjwa kupitia huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani. Kutoka Kushoto ni daktari bingwa wa upasuaji wa Muhimbili, Dkt Godfrey Mchele na mtaalam wa tiba ya radiolojia, Profesa Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani.
Baadhi ya wataalam wa tiba hiyo pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Dkt. Flora Lwakatare.
Wataalam wa radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) pamoja na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani wakishirikiana kuzibua njia ya nyongo ya mgonjwa kupitia huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia.
Mtaalam wa tiba radiolojia, Profesa Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi wataalam wa Muhimbili, MUHAS na MOI walivyofanya maandalizi ya kufanikisha huduma ya tiba radiolojia. Kushoto ni Dkt. Lwakatare na kulia ni mtaalam wa huduma za radiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Emory nchini Marekani.



Hivyo makala WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI

yaani makala yote WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/wagonjwa-23-wapatiwa-huduma-ya-tiba-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI"

Post a Comment