Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni

Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni
kiungo : Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni

soma pia


Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni


Kambi rasmi ya upinzani bungeni imelaani na kupinga vitendo viovu alivyotendewa Mnadhimu wa Kambi hiyo, Tundu Lissu, ambaye alinusurika kifo baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7, mwaka huu mjini Dodoma

Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, anaendelea kupatiwa matibabu katika   hospitali moja ya Nairobi,   Kenya.

Akiwasilisha bungeni maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni jana kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/2019 kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa kambi hiyo,  Halima Mdee, David Silinde alisema vitendo hivyo vinatakiwa vikemewe kwa uzito unaostahili.

Silinde  ambaye ni Mbunge wa Momba (Chadema), alisema vitendo hivyo vikiachwa viendelee bila kukemewa kuna hatari ya kundi linalohisi kuonewa likakosa uvumulivu na hivyo kuathiri amani ya nchi.

“Ingawa  miezi miwili sasa imepita tangu Lissu anusurike kifo baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi wakati mkutano  wa nane wa bunge ukiwa unaendelea na vikao vyake hapa Dodoma na mpaka sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na serikali juu ya kukamatwa kwa watu waliohusika na tukio hilo.

“Ikiwa polisi wameshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata wahalifu hao ndani ya miezi miwili, Kambi Rasmi ya upinzani bungeni  haioni muujiza wowote unaoeweza kutendeka ili watu hao wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria hata kama polisi wataongezewa miezi mingine miwili.

“Tafsiri ya ukimya huo wa serikali ni rahisi, kwamba hakuna dhamira ya dhati wala utayari wa kushughulikia jambo hilo. Hili la kuanza kutuwinda kwa lengo la kutuua, hatuwezi kamwe kulinyamazia,” alisema.

Alisema Kambi Rasmi ya Upinzani inatoa wito kwa wananchi wote kupaza sauti zao kupinga uonevu na ukandamizaji wa haki, kupinga matukio ya utekaji, utesaji na umwagaji wa damu katika nchi.


Hivyo makala Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni

yaani makala yote Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mjadala-wa-tundu-lissu-waibuka-bungeni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni"

Post a Comment