RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE".

RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE". - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE"., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE".
kiungo : RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE".

soma pia


RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE".

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 4 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza kwaajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Mabasi 4 aliyoyakabidhi RC Makonda Leo ni Kati ya Mabasi 11 yaliyokuwa yamekufa (ukweche) ambapo baada ya RC Makonda kuyaona na kubaini uhaba wa magari kwa vyombo vya ulinzi na usalama aliwatafuta wafadhili wa Kampuni ya Dar Coach Ltd waliojitolea kuyarejeshea uhai magari hayo na hatimae leo yanatembea Barabarani yakiwa mazima.

RC Makonda amesema ukarabati wa mabasi hayo ulihusisha Kubadilisha Bodi, kupaka Rangi, kubadili Viti, kuweka Mfumo wa kuchaji simu, AC, TV, Taa,Madirisha, Matairi pamoja na kuongeza na kupunguza idadi ya viti.

Aidha RC Makonda amesema mkakati wa kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama utaendelea ikiwa ni pamoja na kugusa maisha ya mtumishi mmojammoja kwa kuwapatia mikopo ya viwanja vya bei nafuu. Hata hivyo RC Makonda ameshukuru Kampuni ya Dar Coach Tanzania Ltd kwa uzalendo walioonyeaha kukarabati magari hayo pasipo kutumia pesa ya serikali.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Luteni Jenerali Yacoub Mohamed amempongeza RC Makonda kwa ubunifu wa kufufua magari yaliyokuwa yamekufa ambapo ameeleza kuwa yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaongezea ufanisi katika kazi kwa kupunguza changamoto ya usafiri.

Mabasi 4 yaliyokabidhiwa leo ni Ashok Leyland 01, Iveco 2 na Toyota Coaster moja huku magari mengine 7 yakiwa hatua ya mwisho kukamilika.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisalimiana na baadhi ya Maofisa wa jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),wakati alipokwenda leo kukabidhi Mabasi 4 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
 Baadhi ya magari yaliyokabidhi wa kwa JWTZ na Jeshi la Magereza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiagana na mmoja wa Maoisa wa JWTZ,mara baada ya kukabidhi Mabasi 4 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza kwaajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
 Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano hayo
 


Hivyo makala RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE".

yaani makala yote RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE". Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE". mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/rc-makonda-akabidhi-mabasi-4-kwa-vyombo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE"."

Post a Comment