title :
kiungo :
Na Anitha Jonas – WHUSM,Arusha.
Serikali imewataka watanzania kudumisha na kurithisha amali za urithi wa asili wa utamaduni wa kitanzania kwa vijana na watoto kwa manufaa ya kizazi kijacho.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi alipokuwa akifungua Tamasha la Urithi Festival kwa niaba ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Utamaduni Dkt. Harrison Mwakyembe katika uwanja wa Shekhe Amri Abed.
Akiendelea kuzungumza katika sherehe hizo za ufunguzi wa Tamasha hilo Bi.Mlawi asisitiza kuwa uwepo wa tamasha hilo utatoa fursa mbalimbali kwa watanzania wa kunadi,kuonesha na kutangaza rasilimali za utalii wa utamaduni ndani na nje ya nchi.
“Uanuai wa Maendeleo ya sekta ya utalii wa kiutamaduni ili uishi na usiwe katika hatari ya kupotea unahitajika kutambua na kuthamini urithi wa Jadi kama Mila,Desturi,Lugha,Maadii na Imani hivyo uhifadhi,utafiti na utasaidia kunadi kutaendeleza rasilimali za asili za taifa,”alisema Bi.Mlawi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Festival Taifa Prof.Audax Mabula alieleza kuwa wazo la kuanzishwa kwa tamasha hilo lilitokea Wizara ya Maliasili na Utalii lengo likiwa ni kutangaza utalii wa kiutamaduni kwani Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya kiutamaduni ambavyo ni hazina kuwa kwa Taifa.
“Nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vingi vya kiutamaduni kama michoro ya mapangoni inayopatika kama Kondoa,makundi manne ya lugha za afrika yanayopatikana mkoa wa Manyara na jirani,ngoma za asili kutoka makabila mbalimbali nchini pamoja na vyakula vya asili,”alisema Prof.Mabula.
Aidha, nae Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori Tanzania Dkt. James Wakibala alitoa salamu za Waziri wa Maliasili Utamaduni Sanaa na Michezo kwa wadau wa Mkoa wa Arusha na viongozi wake waliyoshiriki tamasha hilo kwa kuwapongeza katika kushiriki tamasha hilo ambalo kwa namna moja litasaidia kuendeleza utalii katika sekta ya Utamaduni.
Hata hIvyo Katibu Mkuu huyo katika hitimisho la hotuba yake aliiomba Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii kushirikiana na Wizara yake katika maandalizi ya tamasha hilo kwa mwakani kwani wote wanadhamana ya kukuza na kutangaza utalii wa Kiutamaduni.
Halikadhali hitimisho la Tamasha hilo kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika Oktoba 13,mkoani hapo na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/na-anitha-jonas-whusmarusha.html
0 Response to " "
Post a Comment