title : MKAKATI KUTOKOMEZA JANI LA GUGU KAROTI LINALOUA WANYAMA,KUPUNGUZA MAZAO WAANZA
kiungo : MKAKATI KUTOKOMEZA JANI LA GUGU KAROTI LINALOUA WANYAMA,KUPUNGUZA MAZAO WAANZA
MKAKATI KUTOKOMEZA JANI LA GUGU KAROTI LINALOUA WANYAMA,KUPUNGUZA MAZAO WAANZA
Na Seif Mangwangi,Arusha
UONGOZI wa shamba la Serikali la kuzalisha aina tofauti za mbegu (ASA), lililopo Ngaramtoni wilayani Arumeru , umeanza mikakati ya kutokomeza jani aina ya Gugu karoti (pyrthrum), ambalo limekuwa likiua wanyama na kupunguza mazao endapo litaingia shambani.
Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa mapambano dhidi ya jani hilo chini ya wajumbe wa kamati ya mkoa ya mapambano dhidi ya jani hilo, Meneja wa shamba hilo la mbegu, Zawadieli Mrinji alisema jani hilo ambalo limeonekana pembezoni mwa mashamba ya mbegu ni hatari na linatakiwa kutokomezwa haraka sana.
Alisema tayari uongozi wa shamba umeanza kupuliza sumu kuua kabisa jani hilo ambalo alisema utafiti unaonyesha limekuwa likisambaa kwa kasi kubwa kufuatia mbegu zake kutawanywa na upepo pamoja na mafuriko.
Mrinji,alisema shamba hilo lina zalisha mbegu mbalimbali zikiwemo Maharage, Mahindi, Alizeti na Ngano ,hivyo inahitajika nguvu ya pamoja na haraka kutokomeza gugu hilo ambalo limeshaonyesha madhara makubwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya mkoa wa Arusha ya kutokomeza gugu karoti Ndelikwa Kaaya alisema kikao hicho kimeitishwa ili kuwa na mkakati wa pamoja wa kuzuia gugu karoti lisiingie kwenye mashamba ya mbegu ya serikali na matokeo yake kuathiri uzalishaji wa mbegu bora .
Alitahadharisha kuwa gugu hilo linaweza kuingia hadi ndani ya hifadhi za taifa ambapo wanyama pori wengi wakiwemo Pundamilia wanauwezekano mkubwa wa kupoteza maisha kwa kula majani hayo.
Kaaya, alisema kuwa kamati yake katika kukabiliana na gugu hilo, imefanikiwa kulifikisha ofisi ya Makamu wa Rais na sasa suala hilo limekuwa ni la kitaifa ambapo tayari serikali baada ya kutambua athari zake imeunda timu maalumu au kikosi kazi kwa lengo la kutokomeza gugu hilo.
Mkurugenzi mstaafu wa kituo cha utafiti wa kilimo SARI, Dk Mbwana Ally,alisema kutokana na watu kutolifahamu gugu hilo wamekuwa wakilitumia kama sehemu ya mapambo kwenye harusi na baada ya hapo mbegu zake huwa zinatupwa hivyo kilichopo sasa ni kuendela kuelimisha wananchi ngazi mbalimbali ili kulitokomeza.
Wakichangia katika kikao hicho wadau wengi walionyesha wasi wasi wa Gugu karoti kuingia kwenye hifadhi za taifa za Ngorongoro na Serengeti na hivyo linaweza kuathiri shughuli za utalii kwa asilimia 60 hadi 70 iwapo hakutakuwepo na juhudi kubwa za kulitokomeza .
Katika utafiti uliofanywa na taasisi ya TPRI gugu hilo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya binaadam ikiwemo Kansa ,kupatwa na mzio wa ngozi, kuathiri uzalishaji wa mazao na kuathiri mifugo.
Wamesema gugu hilo hivi sasa limeshaenea katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Kagera na Geita.
Meneja wa shamba la kuzalisha mbegu ASA, Zawadiel Mrinji akimuonyesha mmoja wa wadau jani aina ya gugu karoti linavyokua kwa kasi pembezoni mwa barabara ya Arusha -Namanga wakati wa zoezi la kung'oa jani hilo.
Gugu Karoti linavyokua kwa kasi pembezoni mwa barabara ya Arusha -Namanga wakati wa zoezi la kung'oa jani hilo.
Hivyo makala MKAKATI KUTOKOMEZA JANI LA GUGU KAROTI LINALOUA WANYAMA,KUPUNGUZA MAZAO WAANZA
yaani makala yote MKAKATI KUTOKOMEZA JANI LA GUGU KAROTI LINALOUA WANYAMA,KUPUNGUZA MAZAO WAANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKAKATI KUTOKOMEZA JANI LA GUGU KAROTI LINALOUA WANYAMA,KUPUNGUZA MAZAO WAANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mkakati-kutokomeza-jani-la-gugu-karoti.html
0 Response to "MKAKATI KUTOKOMEZA JANI LA GUGU KAROTI LINALOUA WANYAMA,KUPUNGUZA MAZAO WAANZA"
Post a Comment