title : Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti.
kiungo : Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti.
Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti.
NaLilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali imetoa kibali cha kuajiri watumishi wapya 15,000 ili kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi wa Umma waliobainika kughushi vyeti.
Hayo yameelezwa leo Bunge, Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Capt. (Msataafu) George Mkuchika alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Aida Khenani kuhusu mkakati wa Serikali wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliokumbwa na sakata la vyeti feki.
"Vibali vya kuajiri watumishi hao vimetolewa katika ngazi ya Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waajiri wote wameendelea kujaza nafasi hizo, " alisema Mhe. Mkuchika.
Vilevile, amesema Serikali imetoa vibali vya ajira kwa Mamlaka zote za Serikali za Mitaa Kumb. Na. CFC.26/205/01/PF/91 cha tarehe 22 Agosti, 2017 na kibali Kumb. Na CFC.26/205/01/GG/95 cha tarehe 12 Machi, 2018 kuziba nafasi zote za Watendaji wa Vijiji na Mtaa zilizoachwa wazi kutokana na zoezi la kuhakikiwa vyeti kwa kuajiriwa watumishi wapya.
Aidha, amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa kutambua umuhimu kwa kuajiri watumishi wa kada mbalimbali Serikali imetoa vibali vya kuajiri watumishi 22, 150 wakiwemo watumishi wa kada za Ualimu 6,840, Fundi Sanifu wa Maabara za shule 160, kada za Afya 8,000, Wahadhiri wa Vyuo Vikuu 624 na watumishi 6,526 wa kada nyingine.
Hivyo makala Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti.
yaani makala yote Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/serikali-imetoa-kibali-cha-ajira-15000_10.html
0 Response to "Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti."
Post a Comment