title : NDIKILO AIELEKEZA HALMASHAURI YA MAFIA KUWATUMIA WAWEKEZAJI KUINUA MAPATO
kiungo : NDIKILO AIELEKEZA HALMASHAURI YA MAFIA KUWATUMIA WAWEKEZAJI KUINUA MAPATO
NDIKILO AIELEKEZA HALMASHAURI YA MAFIA KUWATUMIA WAWEKEZAJI KUINUA MAPATO
NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA
MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,ameielekeza halmashauri ya Mafia kukaa meza moja na baadhi ya wawekezaji wilayani humo ili kuangalia namna ya kulipa kodi itakayosaidia kuondoa udumazi wa mapato kwenye halmashauri hiyo.
Pamoja na hilo ,amewataka watanzania kuacha kuchagua kazi ,bali watumie fursa ya viwanda vingi vinavyojengwa kupata ajira .
Mkuu huyo wa mkoa huo aliyasema hayo ,wakati kamati ya siasa ya mkoa ilipokwenda kutembelea uwekezaji mkubwa wa shamba la ufugaji samaki aina ya kamba katika kiwanda cha Alpha Crust .
Alisema ,uwekezaji huo ni mkubwa ambao umegharimu dollar za Kimarekani milioni 15 sawa na sh. bilioni 32 za Kitanzania ,hivyo ni lazima uungwe mkono kwani ni moja ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika sekta ya uvuvi .
Aidha, aliitaka uhamiaji pamoja na idara ya kazi kuacha urasimu katika kutoa vibali vya kuishi na vya kazi kwa wataalamu mbalimbali kutoka nje ya nchi ,wanaokuja kwa ajili ya kusimamia uzalishaji katika viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo (mwenye shati la kijani)akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Alpha Crust (wa kwanza kushoto) na wa pili kutoka kulia ni Katibu tawala Mkoa wa Pwani (RAS).(Picha na Mwamvua Mwinyi) 
Hivyo makala NDIKILO AIELEKEZA HALMASHAURI YA MAFIA KUWATUMIA WAWEKEZAJI KUINUA MAPATO
yaani makala yote NDIKILO AIELEKEZA HALMASHAURI YA MAFIA KUWATUMIA WAWEKEZAJI KUINUA MAPATO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NDIKILO AIELEKEZA HALMASHAURI YA MAFIA KUWATUMIA WAWEKEZAJI KUINUA MAPATO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/ndikilo-aielekeza-halmashauri-ya-mafia.html
0 Response to "NDIKILO AIELEKEZA HALMASHAURI YA MAFIA KUWATUMIA WAWEKEZAJI KUINUA MAPATO"
Post a Comment