title : Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’
kiungo : Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’
Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’
Mjadala Mkali wa kujadili Ripoti ya kamati ya fedha katika Bunge la NNE la Afrika Mashariki,EALA umeendelea Jana huku wabunge mbalimbali wakiendelea kumtupia lawama katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC,Liberat Mfumukeko kuwa ndo chanzo cha ubadhidifu wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 10 za jumuiya hiyo.

Katika kikao hicho Mbunge wa Kenya Simoni Mbugua alitishia kujihudhulu nafasi yake ya ubunge iwapo wahusika hawatachukuliwa hatua za kinidhamu.

“Katibu Mkuu kwa muda mrefu amekuwa akifuja fedha na si pesa kidogo ukijumlisha fedha ambazo zimepotea ni zaidi ya dola Milioni 10″Amesema.

Amesema fedha hizo zinatoka kwa wachuuzi wa nchi wanachama ili zitumike kwa watu wa EAC lakini zimekuwa zikipotelea Mifukoni mwa wachache bila sababu za msingi

“Fedha hizo zikitolewa zinakuja zinaporwa na Katibu Mkuu na watu wake, wanapora na kuweka kwenye mifuko yao ,Kwenye Masoksi wanabeba pesa zote ,sasa mwananchi aliyeko kule anajua mambo yanaenda vizuri lakini sisi kama wabunge tunasema inatosha ,hatutakubali tena” Amesema Mbugua

Aidha alisema kuwa yeye kama Mbunge afadhali atoke kwenye nafasi yake kuliko kuona jumuiya ikiharibiwa kwa kiasi hicho.

Aliongeza kuwa kulitaka Bunge hilo kuiga utendaji wa Rais John Magufuli na Rais Kenyatta wa Kenya ambao wameonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na ufisadi kwa kuwafunga watuhumiwa wanaopatika na hatia.
Hivyo makala Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’
yaani makala yote Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/wabunge-eala-wacharuka-dola-milioni-10.html
0 Response to "Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’"
Post a Comment