title : Makamu wa Rais ataka Uchunguzi Majengo Mapya Chuo Cha Misitu OLMOTONYI..Tizama Picha
kiungo : Makamu wa Rais ataka Uchunguzi Majengo Mapya Chuo Cha Misitu OLMOTONYI..Tizama Picha
Makamu wa Rais ataka Uchunguzi Majengo Mapya Chuo Cha Misitu OLMOTONYI..Tizama Picha

Makamu wa Rais Nchini Mama Samia Suluhu ametaka uchunguzi ufanyike katika Mradi wa ujenzi wa Majengo mawili ya Bweni la Kike na ukumbi wa Mihadhara katika chuo cha Misitu Olmotony wilaya ya Arumeru yaliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.8 Fedha kutoka ufadhili wa Nchi ya Norwey.
Akiongea Jana katika chuo hicho kilichopo Arumeru Mkoani Arusha, wakati alipokuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa majengo hayo,Makamu wa Rais alisema kuwa utaratibu wa serikali kwa sasa ni kujiridhisha na klmatumizi ya fedha iliyotumika ,hivyo lazima tathimini ifanyike ili kujiridhisha na kiasi cha fedha iliyotumika katika ujenzi wa majengo hayo.
"Kwa Macho ukiangalia majengo haya yanaonekana ni Mazuri na imara ingawa kwa siku hizi tunavyofuatila kila.senti iliyotumika lazima tufanye tathimini ili kujiridhisha na kiasi cha fedha kilichotumika" Amesema Mama Samia
Akizungumzia suala la uhifadhi wa Mazingira ameeleza kuwa serikali ya Tanzania inatambua kuwa uhifadhi ,utunzaji wa mazingira na usimamizi wa mazingira ni suala la kipaumbele kwa maendeleo ya taifa ndio maana serikali inaandaa sera na mikakati ya utunzaji wa mazingira nchini.
Ametaka wizara ya maliasili na Utalii kubuni miradi mingi zaidi itakayonufaisha sekta ya utalii kama mradi unaofadhiliwa na serikali ya Norway katika wilaya 12 hapa nchini.
Amehimiza wizara hiyo kuendelea kukienzi kukiimarisha na kuboresha mifumo ya chuo hicho ili iendane na kasi ya karne ya 21 hususani katika suala zima la matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ili chuo hicho kiendelee kutoa mafunzo kikamilifu kuboresha mifumo kuende sambamba na kuboresha miundo mbinu kuwajengea wakufunzi uwezo na kuongeza vitendea kazi.
Kwa upande wake Naibu waziri wa maliasili na Utalii Japhet Hasunga amesema Kuwa kasi kubwa ya uharibufu wa misitu hapa nchi inazidi kushika kasi kutokana na matumizi makubwa ya Misitu yanayofanywa na binadamu na kufikia asilimia 90.
Amesema kuwa mchango mdogo wa sekta hiyo ya misitu na nyuki ndio maana wizara hiyo imekuja na mkakati huo wa kuboresha chuo cha misitu Olmotonyi ili kuongeza wafanyakazi katika sekta hiyo lengo sekta hiyo isaidie kukuza mapato.
"Chuo hiki kwa sasa kinajumla ya wanafunzi 600 ila mahitaji yake ni kudahili wanafunzi 1000 ambao watatosheleza kushughulikia suala la uhifadhi wa mazingira na kupunguza changamoto iliyopo" Amesema Hasunga
Naye Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa Nchi inahitaji takwimu sahihi za ukubwa wa tatizo la uharibufu wa mazingira ambapo asilimia 61 ya nchi ipo katika hatari ya kuwa jangwa.
Amesema kuwa uchumi wan chi unalazimika kwa kulindwa kwa kuhifadhi rasilimali na misitu iliopo hapa nchini katika kuhakikisha tunaepuka na mabadiliko ya tabianchi.
Hivyo makala Makamu wa Rais ataka Uchunguzi Majengo Mapya Chuo Cha Misitu OLMOTONYI..Tizama Picha
yaani makala yote Makamu wa Rais ataka Uchunguzi Majengo Mapya Chuo Cha Misitu OLMOTONYI..Tizama Picha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Rais ataka Uchunguzi Majengo Mapya Chuo Cha Misitu OLMOTONYI..Tizama Picha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/makamu-wa-rais-ataka-uchunguzi-majengo.html
0 Response to "Makamu wa Rais ataka Uchunguzi Majengo Mapya Chuo Cha Misitu OLMOTONYI..Tizama Picha"
Post a Comment