SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI

SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI
kiungo : SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI

soma pia


SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI

Yasema wasipojirekebisha italivunja baraza lao

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 30 kwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kujirekebisha na kumaliza tofauti zao ndani ya siku 30 na iwapo wataendelea na vurugu Serikali haitosita kuvunja baraza la Madiwani.

Amesema hatua hiyo inatokana na Madiwani hao kutumia muda mwingi wakigombana badala ya kuwahudumia wananchi, Serikali inataka kuona wananchi wakihudumiwa kwa kuboreshewa maendeleo katika maeneo yao na si kushuhudia viongozi wakigombana kwa maslahi binafsi. 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Julai 28, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kigoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenye uwanja wa Kawawa, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kigoma.

“Serikali hairidhishwi na utendaji wenu na nimewapa muda wa mwezi mmoja kumaliza tofauti zenu. Nataka muendelee kufanya kazi za kuwatumikia wananchi wa Manispaa hii ambao wamewachagua ili muwatatulie kero zao na si kuendeleza migogoro,” amesisiza.

Amesema Madiwani hao wanatakiwa kufuatilia changamoto zinazowakabili wananchi wao ikiwemo ya upatikanaji wa dawa katika hospitali, zahanati na vituo vya afya, ambapo licha ya Serikali kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa lakini bado wananchi wanaendelea kukosa huduma hiyo.

Waziri Mkuu amesema matatizo ya madiwani wa Manispaa hiyo anayafahamu na iwapo watashindwa kujirekebisha Serikali haitosita kulivunja baraza hilo kwa sababu Madiwani wake wanatumia muda mwingi kugombana badala ya kuwahudumia wananchi.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa mkoa wa Kigoma kwamba Serikali itaboresha miundombinu ya mkoa huo ikiwemo ya reli, barabara, ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege utakaokuwa na uwezo wa kutua ndege kubwa.

Amesema lengo la maboresho hayo ni kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha biashara utakaounganisha nchi za Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Burundi kwa kuimarisha vivutio vya uwekezaji.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JULAI 28, 2018.
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza Mkutano wa Wadau wa Michikichi kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma Julai 28, 2018. Kulia ni mkewe Mary na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga. 
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza Mkutano wa Wadau wa Michikichi kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma Julai 28, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba.
Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Michikichi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoongoza mkutano huo kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma Julai 28, 2018.


Hivyo makala SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI

yaani makala yote SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/serikali-yatoa-siku-30-kwa-madiwani-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA MADIWANI WA KIGOMA UJIJI"

Post a Comment