title : TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017
kiungo : TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017
TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya Utunzaji bora wa Mahesabu na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), baada ya kufanya Vizuri kwenye kada hiyo katika Mwaka wa fedha 2016/2017.
Akipokea tuzo hiyo Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa TANESCO, Bi RENATA NDEGE ameishukuru Bodi ya Wahasibu na wakaguzi (NBAA), kwa kutambua Utendaji Kazi wa Shirika hilo la Ugavi wa umeme hapa Nchini.
" Napenda kuishukuru Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi kwa kuonesha imani katika Utendaji kazi wetu hususani kwenye Kada hii ya Masuala ya Utunzaji wa fedha, Sisi kama Idara tunaahidi Kuimarisha Utendaji Kazi wa TANESCO kwa Kushirikiana na NBAA" alisema Bi RENATA.
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Fedha katika Shirika la Umeme (TANESCO), wakionekana kufurahia tuzo waliyokabidhiwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu, wameuambia Mtandao wa www.habari360.co.tz kwamba Wataendelea Kuchapa kazi Kwa weledi ili Kulisaidia Shirika Kutimiza Majukumu yake kwa Umma wa Watanzania.
Tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa Idara ya Fedha ya Shirika la Umeme (TANESCO), imeakisi Ubora wa Shirika hilo la Umma katika Utunzaji wa Mahesabu ya Fedha.
Hivyo makala TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017
yaani makala yote TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/tanesco-yakabidhiwa-tuzo-ya-utunzaji.html
0 Response to "TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017"
Post a Comment