DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF

DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF
kiungo : DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF

soma pia


DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ameshauri Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) uanzishe kazi za ajira za muda, kwa walengwa wa Mpango huo kutoka jamii ya Wahadzabe waliopo Wilayani Mkalama ili uwasaidie kuinua uchumi wao.

Dkt Nchimbi ametoa ushauri huo mara baada ya kutembela kijiji cha Singa Wilayani Mkalama na kuona bwawa litakalotumika kuhifandhi maji ya mvua kwa ajili ya shughuli mbalimbali lililojengwa na walengwa wa Tasaf Kijijini hapo kisha kutembelea kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza Wilayani humo aliposhuhudia malipo ya walengwa wa kihadzabe wa Mpango wa Tasaf.

Ameeleza kuwa jamii ya wahadzabe hawana mradi unaohusisha kazi za ajira za muda ambazo zimekuwa zikisaidia katika kuongeza kipato, kuwafundisha thamani ya kazi pamoja na kutekeleza miradi ambayo imekuwa ikisaidia jamii nzima kama vile mabwawa na barabara.

“Nashauri TASAF kabla ya msimu huu wa mvua kuisha muwaletee na hawa wahadzabe mradi wa ajira za muda kama ambavyo walengwa wa vijiji vingine wamekuwa wakifanya kazi hizo na zimekuwa zikichangia maendeleo kwa vijiji vyao”, ameeleza na kuongeza kuwa,

“Miradi ya ajira za muda zitawafundisha Wahadzabe kujituma kufanya kazi ambazo zinachangia maendeleo ya jamii huku kazi hizi zikiwa kama darasa la wao kujifunza kwa vitendo kuwa kama anaweza kwa mfano kushiriki kujenga bwawa basi anaweza kufanya jambo kubwa katika familia au maisha yake”, amesisitiza Dkt Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na Wahadzabe waliokuwa wakijiandaa kupokea fedha kutoka Mpango wa Tasaf katika kijiji cha Munguli Wilayani Mkalama, Dkt Nchimbi amewatahadharisha kutofanya matumizi mabaya ya fedha hizo.
Walengwa wa Tasaf wa kijiji cha Singa Wilayani Mkalama wakimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (hayupo pichani) alipowatembelea kushuhudia ujenzi wa bwawa walilolijenga katika mpango wa ajira za muda za Tasaf.
Bwawa lililopo katika kijiji cha Singa Wilayani Mkalama lililojengwa na walengwa 246 wa Tasaf katika mpango wa ajira za muda, bwawa hilo linaujazo wa mita 5777.6 ambalo litasaidia upatikanaji wa maji na uanzishwaji wa kilimo cha umwagiliaji, Dkt Nchimbi ameagiza halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kuweka miundombinu ya kunyweshea maji mifugo kutoka katika bwawa hilo.



Hivyo makala DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF

yaani makala yote DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/dkt-nchimbi-ashauri-wahadzabe-wapewe.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF"

Post a Comment