title : CCM WAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA
kiungo : CCM WAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA
CCM WAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Chama cha mapinduzi kimesema kuwa kipo kwa ajili ya kuwatumikia na kusikiliza shida za wananchi na wamejipanga kuhakikisha wanaisimamia serikali ipasavyo ili ilani ya chama hicho inatekelezwa kwa asilimia zote na serikali inayoongozwa na chama hicho.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya ccm katika kata ya Kaloleni jijini Arusha Naibu Katibu mkuu wa ccm Bara Rodrick Mpogoro amesema kuwa wakazi wa jiji la Arusha wanategemea sekta ya utalii na jiji hilo ni kitovu cha utalii ndio maana ccm chini ya serikali inayoongozwa na chama hicho ikaona hilo na kuamua kufufua shirika la ndege ili watalii waje moja kwa moja na kusaidia mkoa huo kukua kiuchumi.
Amesema kuwa mgombea wa chama cha mapinduzi kwenye kata hiyo atasaidia ukuaji wa maendeleo kwa wananchi na kuhakikisha kuwa malengo ya huduma bora yanawafikia wananchi kwa kasi badala ya hapo awali kwani chama hicho kimejipanga kuhakikisha wanashinda chaguzi mbali mbali kama hapo awali.“Najua Teyari wagombea 12 wa ccm wanasubiria kuapishwa kati ya wagombea 20 hivyo hawa 8 ninaimani kuwa nao watapigiwa kura na chama chetu kuendelea kupata ushindi katika uchaguzi huu”alisema Mpogoro
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka alisema anayoimani na chama hicho kushinda uchaguzi kwani teyari dalili zinaonyesha kuwa chama hicho teyari kimeshinda kwa kishindo uchaguzi huo.Amesema kuwa wakati akimndai mgombea urais wa ccm 2015 kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid aliwaambia huyu ndio rais lakini wengi walimshangaa na kuona kinyume kwa mapenzi yao lakini sasa wanaona yale aliyowaeleza na wengi wanakubaliana na kauli hiyo.
“Najua wengi mmesahau wakati ule wa kampeni ya urais leo nakuja tena hawa wanaorudi ccm sio bahati mbaya hata mgombea wa ukawa 2015 alishasema upinzani ukishindwa uchaguzi huo wasubiri miaka 50 sasa wenyewe mnaona hilo linajitokeza kwa sababu alitambua mgombea wa ccm ni mtu muadilifu na anafanyakazi kile anachoamini kwa maslahi ya wanyonge”alisema sendeka
Nae Moja wa wananchi wa Kaloleni na Kada wa chama hicho John Mshana amesema kuwa anaamini wagombea waliotoka chadema wameaacha maslahi mapana na kuamua kuona wananchi waliowachagua ndio wenye maamuzi na wao kurudi ccm kwa maslahi mapana ya wananchi kuwatumikia kwa mapana badala ya huko walikokuwa awali.
Amesema kuwa kulikuwa na mtu mmoja alikuwa mjanja sana akamshika kipepeo na kumuuliza mwenzake mjanja huyu kipepeo amekufa au yu hai basi Yule mwezake alijibu kuwa uhai wa kipepeo upo mikononi mwako ndio hawa wagombea wetu uhai na maendeleo ya wananchi yapo mikononi mwao kwa sasa.
Hivyo makala CCM WAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA
yaani makala yote CCM WAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM WAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/ccm-wazindua-kampeni-za-udiwani-arusha.html
0 Response to "CCM WAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA"
Post a Comment