title : WANAJESHI JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN
kiungo : WANAJESHI JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN
WANAJESHI JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN
Na Luteni Selemani Semunyu
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kikosi cha 11 wametakiwa kujivunia mafanikio yaliyopatikana kufuatia utumishi wao uliotukuka kwa kipindi cha Mwaka Mmoja waliokuwa wakishiriki Ulinzi wa amani Jimboni Darfur nchini Sudan na kutunukiwa Nishani ya umoja wa Mataifa.
Hayo yalibainishwa na mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID jimboni Darfur Luteni Jenerali Leonard Ngondi wakati wa sherehe za kuwatunuku Nishani Askari wa JWTZ katika sherrehe zilizofanyika Khor Abeche na kuhudhuruliwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serkali ya Sudan.
“ Kutunukiwa nishani ni jambo la Kujivunia kwa kuwa zimetolewa kwa sababu Askari wamefanya kazi Nzuri amabayo inapaswa kupongezwa hasa kutokana na Doria zilizofanyika ikiwemo katika safu za Milima ya jaber ambayo inakaliwa na Waasi” Alisema Luteni Jenerali Ngondi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Operesheni ya Jaber Mara Lameck Kawiche alitoa wito kwa Wanajeshi wa Tanzania kuendeleza utayari wao ili kuhakikisha wanalinda heshima ya jeshi hilo kwa kufanya kazi kwa Weledi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama ilivyotokea Nchini Kongo.
“ Najivunia Utimamu wa jeshi la Tanzania tuna kila sababu kumpongeza Rais na Amiri Jeshi kwa kuridhia Majeshi ya tanznia Kushiki Operesheni za Umoja wa Mataifa sambamba na Mkuu wa Majeshi kya Ulinzi kwa mafunzo kwa Wanajeshi Wake” Alisema Kawiche.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi UNAMID Jimboni Darfur Sudan, Luteni Jenerali Leonard Ngondi ( wa Tatu kushoto) akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Khor Abeche katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani kutoka Tanzania Hivi karibuni wa nne Kushoto ni kamanda wa kikosi cha Tanzania Kanali Wiliam Sandy .(Picha na Luteni Selemani Semunyu.
Kamanda Kikosi cha Tanzania TANZBATT 11 Jimboni Darfur nchini Sudan, Kanali William Sandy kulia akivishwa nishani na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi UNAMID. Luteni Jenerali Leonard Ngondi katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani kutoka Tanzania Hivi karibuni.(Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Mnadhimu Mkuu wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID akivisha nishani walinda Amani kutoka Tannzaia katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani kutoka Tanzania hivi karibuni katika eneo la Khor Abeche(Picha na Luteni Selemani Semunyu).KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANAJESHI JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN
yaani makala yote WANAJESHI JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAJESHI JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/wanajeshi-jwtz-watunukiwa-nishani-za.html
0 Response to "WANAJESHI JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN"
Post a Comment