SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU

SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU
kiungo : SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU

soma pia


SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua idadi ya Wananchi waliofika kupata huduma wakati alipofanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu salama jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua jokofu la kuhifadhia sampuli ya Damu pindi alipofanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu salama jijini Dar es salaam. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mpango wa Taifa wa Damu salama, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mashine yakupima Sampuli za Damu, Mpango wa Taifa wa Damu salama, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akiongea na Watumishi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu katika taasisi hiyo. 
Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Dkt. Magdalena Lyimo, akisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha) wakati wa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu. 
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kumaliza ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.
………………………. 


Na WAMJW – DSM 

Mpango wa Taifa wa Damu salama imetakiwa kuhakikisha Hospitali Binafsi zote zinaanza kuchangia gharama za huduma za afya ili kupata mgao wa damu. 

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara ya kukagua mashine za kupima sampuli za damu na utendaji kazi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama. 

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa ni lazima Mpango huyo uhakikishe unajiendesha wenyewe na kuhakikisha unapunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali katika kutimiza majukumu yake. 

“Ni lazima kupunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali kwa kuanzisha mfumo wa uchangiaji gharama za huduma za Afya wakati Sera inaelekea kukamilika, Mpango unapendekeza kurudisha gharama kutoka Hospitali binafsi kupitia njia ya Bima” Alisema Dkt. Ndugulile 

Dkt. Ndugulile alisema kuwa Idadi kubwa ya wanaokuja kuchukua Damu katika Taasisi hiyo ni Hospitali Binafsi ukilinganisha na Hospitali za Umma, ambapo mfumo wake ni wakutoza huduma kwa Wananchi (Biashara) 

“Wanaokuja kuchukua Damu nyingi hapa, wengi ni Hospitali Binafsi, kuliko hata za kwetu za umma, Damu nyingi tunawapa, lakini hawa tukiwapa Damu hizi, wao wanaenda wanatoza pesa, kwahiyo sisi tunawatengenezea bidhaa bure halafu wao wanaenda kutoza pesa, hata senti tano sisi hatupati, sio sahihi” alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha, Dkt. Ndugulile amewaagiza viongozi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuangalia ni namna gani Damu iwe ni moja ya vitu vitakavyo gharamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. 

“Muwahusishe Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kuangalia jinsi gani damu itakuwa inagharamiwa na Bima ya Afya, mtuletee mapendekezo na sisi tutafanya maamuzi” Alisema Dkt. Ndugulile. 

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameagiza kufanya maboresho ya mfumo wa Takwimu kuanzia kwenye ukusanyaji wa mapato mpaka hatua ambayo mgonjwa anapata damu hiyo jambo litakalosaidia kuboresha huduma kwa wananchi. 

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameagiza kuweka mikakati ya kuhakikisha wanawabakishia wachangiaji Damu ambao wanakuja kuchangia, hii inatokana na takwimu kuonesha Wachangiaji wa Damu wa hiari wanapungua kutoka 67% mpaka 63% mwaka 2017-2018. 

“Taarifa yenu ya Mwaka 2017-2018 inaonesha kwamba, wachangiaji Damu wa hiari wanapungua kutoka 67% mpaka 63% , maana yake bado kuna changamoto, na kuna kazi tunatakiwa kufanya ikiwemo kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba tunaowapata Mara ya kwanza kuendelea kuwa nao” Alisema Dkt. Ndugulile 

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Dkt. Magdalena Lyimo amesema kuwa Mpango una mkakati wa kuboresha mfumo wa ukusanyaji taarifa na Takwimu za kielektroniki unaunganishwa nchi nzima ili kuleta tija na ubora wa huduma za damu salama nchini. 

Kwa upande mwingine Dkt. Lyimo amesema kuwa Mpango umefanikiwa katika kipindi cha Mwaka 2018 kwa kushirikiana na timu za Mikoa na Halmashauri ulikusanya jumla ya chupa 307,835 ambayo ni sawa na Chupa 6 kwa kila watu 1000, huku Shirika la Afya Duniani linapendekeza kukusanya chupa 10 kwa kila watu 1000, makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la chupa 73,882 sawa na 32% ikilinganishwa na Takwimu za 2017. 

Dkt. Magdalena Lyimo aliendelea kusema kuwa kwa Mwaka 2018, Wastani wa chupa 25,653 zilikusanywa kila mwezi na damu zote zilipimwa magonjwa ya HIV,Kaswende pamoja na makundi ya damu, huku matarajio ni kuongeza damu hadi kufikia chupa 375,000 kwa Mwaka 2019.


Hivyo makala SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU

yaani makala yote SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/serikali-yazitaka-hospitali-binafsi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU"

Post a Comment