title : Muhimbili Yapandikiza Figo Wagonjwa Wanne
kiungo : Muhimbili Yapandikiza Figo Wagonjwa Wanne
Muhimbili Yapandikiza Figo Wagonjwa Wanne
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kupandikizia figo wagonjwa wa nne ikiwa ni mara ya pili kutoa matibabu hayo ya ubingwa wa juu nchini.
Upasuaji huo umefanywa na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India na umekua na mafanikio makubwa kwani wagonjwa wote hali zao zinaendelea vizuri .
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Museru amesema Novemba mwaka jana Muhimbili iliweka historia kwa kufanya upasuaji mkubwa na wa kwanza nchini kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano za kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Akifafanua amesema upasuaji huo wa figo ukifanyika nchini unagharimu Shilingi Milioni 21 na endapo mgonjwa akipelekwa nchini India matibabu yake yanagharimu Shilingi Milioni 80 hadi Shilingi milioni 100.
“Shughuli hii inatuonyesha kwamba hospitali sasa inaweza kupandikiza figo na lengo letu ni kuhakikisha huduma hii inakua endelevu ili kuokoa fedha za serikali kupeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi na pia kuwafikia Watanzania wengi ambao wanahitaji kupandikizwa figo,’’amesema Profesa Museru.
Amesema Hospitali ya Muhimbili itaendelea na shughuli hiyo na kwamba kila mwezi itapandikiza figo kwa wagonjwa watano hivyo kwa mwaka itafanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 60.
Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya BLK ya India wakimpandikiza figo mgonjwa baada ya ndugu yake kutoa figo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo na Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Isaack Mlatie na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo na Upasuaji wa Hospitali ya BLK, Dkt. Ankur Arya. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo na Upasuaji wa Hospitali ya BLK India, Dkt. H. S. Bhatyal wakiendelea na upandikizaji figo kwa mgonjwa.
Wataalamu wakiaandaa figo baada ya kuitoa kwa mchangiaji kabla ya kuipandikiza kwa mgonjwa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo na Upasuaji wa Hospitali ya BLK India, Dkt. H. S. Bhatyal (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wengine baada ya kutoa figo kwa mchangiaji.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Muhimbili Yapandikiza Figo Wagonjwa Wanne
yaani makala yote Muhimbili Yapandikiza Figo Wagonjwa Wanne Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili Yapandikiza Figo Wagonjwa Wanne mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/muhimbili-yapandikiza-figo-wagonjwa.html
0 Response to "Muhimbili Yapandikiza Figo Wagonjwa Wanne"
Post a Comment