title : Rais Magufuli aungana na Wakristo kuadhimisha misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Jijini Dar es Salaam
kiungo : Rais Magufuli aungana na Wakristo kuadhimisha misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Jijini Dar es Salaam
Rais Magufuli aungana na Wakristo kuadhimisha misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 01 Aprili, 2018 ameungana na Wakristo wote Tanzania katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Misa hiyo imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Joseph Padre Venance Tegete.
Akizungumza baada ya kukaribishwa na Padre Tegete kutoa salamu, Mhe. Rais Magufuli amewatakia Watanzania wote heri ya Pasaka na ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuishi kwa amani na upendo huku wakishiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa.
“Kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo ukafufue matendo yetu, tuendelee kuijenga amani yetu, upendo wetu na tujenge maendeleo ya Watanzania wote, kwani Kristo alifundisha upendo miongoni mwetu.
“Kwa hiyo Baba nakushukuru sana kwa kuongoza Misa hii, naomba ufikishe shukrani zangu kwa Kardinali Pengo, Maaskofu wote na Watanzania wote tuendelee kusimama pamoja ili kulijenga Taifa letu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli aliongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam
01 Aprili, 2018
Hivyo makala Rais Magufuli aungana na Wakristo kuadhimisha misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Jijini Dar es Salaam
yaani makala yote Rais Magufuli aungana na Wakristo kuadhimisha misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Jijini Dar es Salaam Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli aungana na Wakristo kuadhimisha misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Jijini Dar es Salaam mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/rais-magufuli-aungana-na-wakristo_1.html
0 Response to "Rais Magufuli aungana na Wakristo kuadhimisha misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Jijini Dar es Salaam"
Post a Comment