title : WAFANYA BIASHARA WA VIPODOZI WA KARIAKOO: TUMECHOKA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU
kiungo : WAFANYA BIASHARA WA VIPODOZI WA KARIAKOO: TUMECHOKA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU
WAFANYA BIASHARA WA VIPODOZI WA KARIAKOO: TUMECHOKA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa TFDA na wamiliki wa maduka ya vipodozi ya Kariakoo. Waliokaa toka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa za Dawa wa TFDA, Bw. Adonis Bitegeko (wa pili), Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya biashara wa Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Martin Mbwana (wa kwanza) na Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba, Vipodozi na Bidhaa Dawa, Bi Grace Shimwela
Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa za Dawa wa TFDA, Bw. Adonis Bitegeko (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina elekezi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya biashara hao Bw. Martin Mbwana (aliyesimama)akizngumza wakati walipozungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo amesema kuwa "tumechoka kukamatwa mara kwa mara na vipodozi vyenye sumu, mitaji yetu inafilisika, sasa tunahitaji elimu na kuzingatia matakwa ya kisheria” anaongea, wakati alipokuwa akichangia maada"
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya vipodozi ya Kariakoo wakifuatilia mojawapo ya maada.
Na: James Ndege – Dar es Salaam
TFDA imetoa elimu kwa wafanya biashara wa vipodozi zaidi ya 30 wanaomiliki maduka ya jumla na rejareja wa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaaam kwa lengo kuwakumbusha mambo muhimu ya kisheria ya kuzingatia katika kufanya biashara hiyo nchini.
Semina hiyo elekezi iliyoratibiwa na Mamlaka kwa kushirikiana na Uongozi wa wadau hao, imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Margareth Ndomondo-Sigonda uliopo TFDA Makao Makuu leo tarehe 7/9/2018.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa za Dawa wa TFDA, Bw. Adonis Bitegeko, alisema “TFDA kama Taasisi ya Umma, ni rafiki kwa wafanyabiashara wote wakiwemo wa vipodozi, na ipo tayari kusikiliza kushauri na kujenga mazingira rafiki ya kufanya biashara kwa lengo la kupata bidhaa salama, bora na zenye ufanisi ili kulinda afya ya jamii na kuleta maendeleo ya nchi”.
“Wafanya biashara wa vipodozi tuliopo Kariakoo na maeneo mengine, tumechoka kukamatwa mara kwa mara na vipodozi vyenye sumu, mitaji yetu inafilisika, tunapelekwa mahakamani sasa tunahitaji elimu ya namna ya kufanya biashara hii kwa kuzingatia matakwa ya kisheria na si vinginevyo” alisema Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya biashara hao, Bw. Martin Mbwana wakati alipokuwa akichangia mada.
Kwa upande wake, Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba, Vipodozi na Bidhaa Dawa, Bi Grace Shimwela alisema, “Kwa mujibu wa Sheria, hairuhusiwi kuingiza vipodozi au bidhaa zinazodhibiwa na Mamlaka ndani ya nchi au katika soko bila ya kusajiliwa na TFDA. Kabla ya kuingiza bidhaa toka nje ya nchi,, hakikisha una kibali cha TFDA ili kuepusha kuingiza bidhaa ambazo si salama na bora ambazo zitaharibiwa au kurudishwa zilikotoka kwa gharama yako.
Pia wakati wa kufuatilia maombi yenu TFDA hakikisheni mnawasilisha nyaraka stahiki, msighushi vibali wala kufanya udanganyifu wa kodi kwani mambo hayo yatasababisha shehena za mizigo yenu ishikiliwe na kufunguliwa kesi. Ninyi wamiliki mnatakiwa kuwasiliana moja kwa moja na TFDA mkipata changamoto zozote, chukueni tahadhari kwa baadhi ya mawakala wa mizigo wasiyo waaminifu mliowapa dhamana ya kufuatilia uingiaji wa mizigo ya biashara zenu”.
Wafanya biashara hao waliishukuru Mamlaka kwa kuwapa elimu muhimu ambapo waliomba iwe endelevu na ishirikishe makundi mbalimbali ya wafanya biashara wakiwemo mawalaka wa mizigo nchini ili kuepuka kuingiza bidhaa zenye madhara kwa watumiaji. “Badala ya kutegemea bidhaa za nje ya nchi pekee, tumieni fursa iliyopo ya Serikali ya Awamu ya Tano, anzisheni viwanda vya vipodozi na TFDA itasaidia kutoa ushauri ili vikidhi vigezo vinavyotakiwa”, alisema Bw. Adonis Bitegeko.
Hivyo makala WAFANYA BIASHARA WA VIPODOZI WA KARIAKOO: TUMECHOKA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU
yaani makala yote WAFANYA BIASHARA WA VIPODOZI WA KARIAKOO: TUMECHOKA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYA BIASHARA WA VIPODOZI WA KARIAKOO: TUMECHOKA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/wafanya-biashara-wa-vipodozi-wa.html
0 Response to "WAFANYA BIASHARA WA VIPODOZI WA KARIAKOO: TUMECHOKA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU"
Post a Comment