title : PROFESA KITILA MKUMBO AMEWATAKA WADAU WA MAJI KUSHIRIKI KATIKA UTUNGAJI SHERIA MPYAA
kiungo : PROFESA KITILA MKUMBO AMEWATAKA WADAU WA MAJI KUSHIRIKI KATIKA UTUNGAJI SHERIA MPYAA
PROFESA KITILA MKUMBO AMEWATAKA WADAU WA MAJI KUSHIRIKI KATIKA UTUNGAJI SHERIA MPYAA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof esa Kitila Mkumbo amewataka wadau wa maji nchini kushiriki katika utoaji wa maoni kuhusiana na utungaji wa sheria mpya ya maji ili kuweza kudhibiti upotevu wa maji.
Amezungumza hayo katika Ofisi za Dawasa jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa sheria hii mpya itasaidia Mambo mengi ikiwa ni pamoja na udhibiti wa maji ambayo yamekuwa yakipotea kwa asilimia 44 mpaka sasa
Prof Mkumbo amesema wizara inapendekeza kuanzishwa kwa Taasisi maalumu ya kushughulikia miradi ya maji mijini na vijijini yaani Rural Water Agency, Taasisi ambayo imekusudia kuimarisha Jumuia za watumiaji wa maji kwa ngazi za vijiji na miji ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa Taasisi mpya ya Dawasa
Kutunga kwa sheria hii mpya ya maji kutaongeza matamanio kwa watumiaji wa maji na kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama kwa uhakika zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya DAWASA Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka wananchi wa Dar Es Salaam na Pwani kushirikiana na Dawasa katika ufanyaji kazi wake hasa kutoa taarifa punde inapobainika uvujaji wa maji, na kusisitiza kuhusu utungaji wa sheria mpya unapofanyika wananchi watoe maoni ili mchakato uwe na tija kwani sheria hii ina manufaa makubwa kwa wananchi.

Hivyo makala PROFESA KITILA MKUMBO AMEWATAKA WADAU WA MAJI KUSHIRIKI KATIKA UTUNGAJI SHERIA MPYAA
yaani makala yote PROFESA KITILA MKUMBO AMEWATAKA WADAU WA MAJI KUSHIRIKI KATIKA UTUNGAJI SHERIA MPYAA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROFESA KITILA MKUMBO AMEWATAKA WADAU WA MAJI KUSHIRIKI KATIKA UTUNGAJI SHERIA MPYAA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/profesa-kitila-mkumbo-amewataka-wadau.html
0 Response to "PROFESA KITILA MKUMBO AMEWATAKA WADAU WA MAJI KUSHIRIKI KATIKA UTUNGAJI SHERIA MPYAA"
Post a Comment