title : OPARESHENI ZA KUZUIA UHALIFU ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
kiungo : OPARESHENI ZA KUZUIA UHALIFU ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
OPARESHENI ZA KUZUIA UHALIFU ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
Na Lydia Churi-Mahakama ya Tanzania
Viongozi wanaohusika na Oparesheni za kuzuia uhalifu wameshauriwa kufuata na kuzingatia sheria inayoongoza namna ya ukusanyaji wa ushahidi ili kuepuka kuharibu ushahidi kabla haujawasilishwa Mahakamani na kupelekea kesi nyingi kuharibika kwa kukosa ushahidi au Mahakama kushindwa kutoa hukumu zinazoendana na kosa husika.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Uyui alipomtembelea Mkuu wa wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake inayoendelea Mahakama Kuu kanda ya Tabora. 
Akitolea mfano wa Oparesheni za uteketezaji wa dawa za kulevya yakiwemo mashamba ya bangi, Jaji Mkuu amesema ushahidi kuteketezwa bila ya kufuata utaratibu huathiri mienendo ya kesi Mahakamani.
Akizungumzia suala la Maadili ndani ya Mahakama, Jaji Mkuu amewaomba Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa wilaya ambao anawatambua kama walezi wa Mahakama kushirikiana kwa karibu zaidi na Mahakama ili kuhakikisha wanawahudumia wananchi ipasavyo katika suala zima la utoaji wa Haki.
Kuhusu kusogeza huduma za kimahakama karibu Zaidi na wananchi, Jaji Mkuu amesema Mahakama kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inao Mpango wa kuanzisha Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kuwafikia wananchi walio mbali na huduma za kimahakama hasa katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora
Naye Mkuu wa wilaya ya Tabora na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Uyui, Queen Mlozi alimweleza Jaji Mkuu kuwa kwa namna wilaya ya Uyui ilivyokaa kijiografia, wananchi hulazimika kufuata huduma za kimahakama umbali wa Zaidi ya kilometa 150 katoka Loya kwenda Kigwa mkoani Tabora.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala OPARESHENI ZA KUZUIA UHALIFU ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
yaani makala yote OPARESHENI ZA KUZUIA UHALIFU ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OPARESHENI ZA KUZUIA UHALIFU ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/oparesheni-za-kuzuia-uhalifu-zatakiwa.html
0 Response to "OPARESHENI ZA KUZUIA UHALIFU ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA"
Post a Comment