MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA
kiungo : MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA

soma pia


MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA

JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.
Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. 

Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
Kamanda Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Naye Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.

Alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti huyo. 

Alisema kiasi kingine cha fedha kinachunguzwa kubaini kilipo.

Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na juhudi za Serikali katika mapambado dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka pamoja na fedha za umma.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Anthony Bahebe akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kuapamba na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) jijini Mwanza Februari 21, 2018 kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA

yaani makala yote MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/mwenyekiti-wa-halmashauri-ya-misungwi_21.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA"

Post a Comment