Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3

Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3
kiungo : Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3

soma pia


Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3

Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 3.4 mwezi Juni, 2018.
Hayo yameelezwa leo na Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa sensa na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo alipokuwa akitoa taarifa  ya mfumuko wa bei kwa mwezi Julai mwaka huu.
Kwesigabo amesema, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa  mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.
"Kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula, ambapo bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya Julai, 2017 na Julai 2018 ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 9.5, mtama kwa asilimia 17.8, unga wa mihogo kwa asilimia 14.1, matunda jamii ya machungwa kwa asilimia 22.2, maharagwe kwa asilimia 5.8 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.5," amefafanua Kwesigabo.
Ameendelea kusema kuwa ni zaidi ya miaka 15 tangu itokee tarakimu kama hiyo ya mfumuko wa bei ambayo iko vizuri kwa uchumi wa nchi.
Aidha ametaja hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya  nchi za Afrika Mashariki kama ifuatavyo; Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 umeongezeka hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018. Kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.35 kutoka asilimia kutoka asilimia 4.28 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.
Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.




Hivyo makala Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3

yaani makala yote Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mfumuko-wa-bei-wa-taifa-umepungua.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mfumuko wa Bei wa Taifa Umepungua Kufikia Asilimia 3.3"

Post a Comment