title : UHAMIAJI YAWASHIKILIA WATANZANIA TISA KWA KUKWAMISHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIU
kiungo : UHAMIAJI YAWASHIKILIA WATANZANIA TISA KWA KUKWAMISHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIU
UHAMIAJI YAWASHIKILIA WATANZANIA TISA KWA KUKWAMISHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIU
IDARA ya Uhamiaji nchini inawashikilia watanzania 9, ambao ni wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIU) jijini Dar es Saalam kwa madai ya kuzuia maofisa wa idara yao kutofanya kazi yao walipofika chuoni hapo.
Akizungumza na Michuzi Blog, leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Ally Mtanda amesema watu hao tisa wamekamatwa jana kwa tuhuma za kuzuia maofisa wa idara hiyo wasitimize majukumu yao na kwa sasa wanawahoji.
"Watu hao baada ya maofisa wetu jana kufika pale KIU waliamua kuwazuia kwa kufunga milango ili tusipate nafasi ya kufanya kile ambacho kimetupeleka,"amesema.
Hivyo kukamatwa kwa watu hao kunafanya idadi ya wanaowashikiliwa na Idara ya Uhamiaji kufikia 48."Idara ya Uhamiaji inaendelea kuwahoji na kati ya hao wanaoshikiliwa wapo raia wa Nigeria watano, raia wa Congo mmoja, raia wa Uganda 30, raia wa Kenya 3 pamoja na hao raia wa Tanzania 9,"amesema.
Amefafanua Idara ya Uhamiaji itaendelea kukagua vyuo mbalimbali nchini kwani ni agizo la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Alipoulizwa kwanini wameanza na KIU amejibu huo ni mwanzo tu kwani watapita kwenye maeneo mbalimbali.
Hivyo makala UHAMIAJI YAWASHIKILIA WATANZANIA TISA KWA KUKWAMISHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIU
yaani makala yote UHAMIAJI YAWASHIKILIA WATANZANIA TISA KWA KUKWAMISHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UHAMIAJI YAWASHIKILIA WATANZANIA TISA KWA KUKWAMISHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/uhamiaji-yawashikilia-watanzania-tisa.html
0 Response to "UHAMIAJI YAWASHIKILIA WATANZANIA TISA KWA KUKWAMISHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIU"
Post a Comment