Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’

Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’ - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’
kiungo : Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’

soma pia


Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’

Leo January 5, 2017 Mfanyabiashara James Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyodai awali kuwa atawataja.

Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.

“Mwizi ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao wameisababishia serikali hasara ya Trilioni 37, pia nimewapelekea TAKUKURU washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao.” – James Rugemarila

Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Trillion 16. Wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.

Tofauti na hayo Rugemarila pia ameiomba mahakama imkubalie akafanyiwe uchunguzi nchini India kwa sababu anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa miaka 9 sasa huku mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi aliiambia Mahakama kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana.

Kutokana na hatua, Hakimu Simba amesema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia anautaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 19,2018.


Hivyo makala Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’

yaani makala yote Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/rugemarila-amewataja-wezi-wa-fedha-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’"

Post a Comment