MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE

MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE
kiungo : MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE

soma pia


MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE


Mwambawahabari


 Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na  Wazee waishio Makao ya Wazee Sukumahela  Wilayani Manyoni wakati wa ziara take inayoendelea Mkoani Singida.
                                                  .......................................................................
                                                        Na ANTHONY ISHENGOMA

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida kuhakikisha wazee wasiojiweza wanaoishi Makao ya Wazee ya Taifa Sukamahela wanapatiwa vyandarua kwa ajili ya kujikinga na Malaria.

Naibu Waziri Ndugulile ametoa agizo hilo alipotembelea makao hayo yaliyoko nje kidogo ya mji mdogo wa Manyoni kujionea hali halisi ya maisha ya Wazee wasiojiweza.

Dkt. Ndugulile ametoa muda wa wiki mbili kwa Mganga Mkuu Mkoa kutekeleza jambo hilo na kutaka mrejesho wa utekelezaji wa agizo hilo.

"Hili ni kosa ambalo siwezi kulisamehe tuna vyandarua vingi vya  kutosha sioni sababu wazee hawa kulala kwenye vyumba bila vyandarua, nawapa wiki mbili kuhakikisha kila mzee analala kwenye chandarua.," Aliagiza Dkt.Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile  amewataka watendaji wa Idara ya  Afya wa Zahanati ya Sukamahela iliyopo katika eneo la makao  ya Wazee hao kuhakikisha wanakuwa na dawa za kutosha hasa zile maalumu kwa ajili magonjwa ya Wazee.

Makao ya Wazee Sukamahela pamoja na mambo mengine yanayowakabili  na upungufu wa chakula, na wamekili kuchoshwa na ulaji wa aina moja ya mboga hivyo   kutoa ombi lao kwa Naibu Waziri kutatua changamoto hiyo.

Naibu Waziri Ndugulile  amehaidi kushughulikia suala la ukarabati wa majengo chakavu ya yaliyopo katika Makazi hayo.

Kwa nyakati tofauti wazee waishio katika makazi hayo wamelalamikia ukosefu wa umeme katika makazi hayo, dawa za magonjwa ya ukoma na vifaa vidogo vidogo kwa ajili ya usafi na kilimo cha mbogamboga pamoja na miundo mbinu chakavu ya vyoo.

Aidha Dkt.Ndugulile amesema serikali inakusudia kufunga baadhi ya vituo na kuvipanga kikanda ili iweze kudumisha huduma kwa wazee wasiojiweza lakini kugeuza makazi yatakayofungwa kuwa nyumba salama kwa ajili kupambana na vitendo vya kikatili.

Naibu Waziri Ndugulile yupo mkoani Singida kufuatilia utekelezaji wa masuala ya Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Jiko  kinapoandaliwa chakula cha Wazee waishio Makao ya Wazee Sukumahela  Wilayani Manyoni wakati wa ziara take inayoendelea Mkoani Singida.a


Hivyo makala MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE

yaani makala yote MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mganga-mkuu-singida-apewa-wiki-mbili.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE"

Post a Comment