title : WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA
kiungo : WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA
WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wakazi 1,000 wa Manispaa ya Songea wanaoidai fidia ya sh. bilioni 3.8 ya eneo lao ambalo limechukuliwa na kuwa eneo la kiuchumi mkoani Ruvuma (Ruvuma SEZ) kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.
Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Manispaa hiyo.Amesema Serikali ya awamu ya tano inatambua kilio chao ambacho alisema ni cha muda mrefu na kwamba alishawahi kupata ombi maalum kutoka kwa mbunge wao wa zamani, Bw. Leonidas Gama ambaye sasa ni marehemu.
“Alipotoka kutibiwa India alikuaja ofisini kwangu na kunieleza kwamba ana mambo mawili ambayo nikifanya ziara mkoani Ruvuma anaomba niyatafutie ufumbuzi. La kwanza lililkuwa ni hili la fidia kwa wakazi wa Mwengemshindo na la pili lilikuwa ni la ujenzi wa kituo cha mabasi cha mabasi cha mjini Songea,” alisema.
“Leo nimefanya ziara maalum kwa ajili yenu kwa sababu serikali ya awamu ya tano iko kwa ajili yenu na hasa wananchi wanyonge. Na tatizo hili inalijua. Kabla sijafika hapa, nilipita kwenye eneo husika na afisa mipango miji akanionyesha ramani ya eneo lenu hili,” alisema.
Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba eneo hilo limetengwa na Manispaa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ambapo wawekezaji watatu tayari wamekwishajitokeza na wanataka kujenga viwanda vitatu. “Kutakuwa na kiwanda cha kusindika mahindi, kutengeneza pumba za kuku na ng’ombe na mbolea. Kiwanda cha pili kitakuwa ni cha kusindika kahawa na cha tatu kitakuwa ni cha kukamua mafuta ya mbegumbegu,” alisema na kuongeza kwamba reli ya kutoka Mtwara kwenda Mbaba Bay inatarajiwa kupita kwenye eneo hilo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika Manispaa ya Songea leo Desemba 23, 2017 ambako alienda kusikiliza kero yao ya muda mrefu ya kutolipwa fidia.
Mkazi wa Msamala katika Manispaa ya Songea, Bibi Monica Joseph Miti akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mwengemshindo. Bibi Miti aliomba asaidiwe kurejeshewa nyumba yake aliyotapeliwa na mtumishi wa Manispaa hiyo baada ya mumewe kufariki.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Hivyo makala WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA
yaani makala yote WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/waziri-mkuu-awatoa-hofu-wakazi-wa-songea.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA"
Post a Comment