title : SERIKALI YATOA SIKU SABA MKANDARASI WA BWAWA LA RUNGWA-ITIGI, KULETA VIFAA MUHIMU VA UJENZI
kiungo : SERIKALI YATOA SIKU SABA MKANDARASI WA BWAWA LA RUNGWA-ITIGI, KULETA VIFAA MUHIMU VA UJENZI
SERIKALI YATOA SIKU SABA MKANDARASI WA BWAWA LA RUNGWA-ITIGI, KULETA VIFAA MUHIMU VA UJENZI
Mkandarasi anayejenga bwawa la Rungwa katika Halmashauri ya Itigi amepewa siku saba na Serikali Mkoani Singida kuhakikisha anapeleka vifaa muhimu vitakavyoongeza kasi na ufanisi wa ujenzi wa bwawa hilo.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola ametoa agizo hilo mapema jana mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo na kukuta ukiwa katika asilimia 35 wakati ulitakiwa kuwa asilimia 60 huku baadhi ya vifaa muhimu vikikosekana.
Nyamkomola amemueleza Mhandisi mwakilishi wa kampuni ya Proactive Independent Group Ltd Elias Gamba kuwa wananchi wa Rungwa hawana maji na juhudi za serikali kuwapatia maji kupitia mradi huo wenye thamani ya zaidi ya milioni mia saba unatakiwa kufanyika kwa kasi na ufanisi wa hali ya juu.
Ameeleza kuwa baada ya kufanya ukaguzi katika bwawa hilo wamebaini kuwa baadhi ya kazi zimekuwa zikifanywa kwa kasi ndogo kutokana na kutokuwepo kwa mashine na badala yake kazi hizo kufanywa na vibarua huku vifaa vingine vikiwa pungufu tofauti na makubaliano katika mkataba.
Mhandisi wa Maji Mkoa wa Singida Lydia Joseph (aliyevaa kofia nyeupe) akiendelea na ukaguzi wa bwawa la Rungwa-Itigi, nyuma yake ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola akiwa na watendaji wa serikali na wawakilishi wa Mkandarasi wa bwawa la Rungwa wakitembelea eneo la Bwawa hilo mapema jana.
Baadhi ya vibarua wakiendelea na zoezi la kuchanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa ukuta katika bwawa la Rungwa – Itigi, Serikali Mkoani Singida imeagiza kazi hio ifanywe na mashine ili kuleta ufanisi na kasi huku vibarua hao wakitakiwa kuendelea na kazi nyingine katika bwawa hilo.
Sehemu ya Bwawa la Rungwa –Itigi linalojengwa na serikali kwa zaidi ya shilingi milioni mia saba ili kutatua kero kubwa ya maji katika kijiji cha Rungwa.
Hivyo makala SERIKALI YATOA SIKU SABA MKANDARASI WA BWAWA LA RUNGWA-ITIGI, KULETA VIFAA MUHIMU VA UJENZI
yaani makala yote SERIKALI YATOA SIKU SABA MKANDARASI WA BWAWA LA RUNGWA-ITIGI, KULETA VIFAA MUHIMU VA UJENZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATOA SIKU SABA MKANDARASI WA BWAWA LA RUNGWA-ITIGI, KULETA VIFAA MUHIMU VA UJENZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/serikali-yatoa-siku-saba-mkandarasi-wa.html
0 Response to "SERIKALI YATOA SIKU SABA MKANDARASI WA BWAWA LA RUNGWA-ITIGI, KULETA VIFAA MUHIMU VA UJENZI"
Post a Comment