Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika

Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika
kiungo : Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika

soma pia


Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika



Wanariadha wakichuana vikali mbio za Nyika, Viwanja vya Magereza ,Kisongo Jijini Arusha. Picha na Gadiola Emanuel.
 

Na Yasinta Amos, Arusha
MKOA wa Arusha umeendelea na maandalizi yake katika mashindano ya mbio za nyika kusaka wanariadha watakaounda timu ya mkoa itakayochuana kitaifa hapo Mwakani.
Ikiwa ni Mara ya pili sasa zoezi la kusaka wanariadha hao likifanyika katika viwanja vya Magereza ambapo wanariadha kutoka vilabu mbalimbali wameonekana kuchuana vikali .
Mshindi kwa upande wa wanaume Josephat Joshua alishinda kwa muda wa wa 29:13:84 akifuatiwa na Silvester Simon Naali muda wa 29:21:70 wote kutoka timu ya klabu ya Polisi na nafasi ya tatu kumwendea mwanariadha Francis Damiani kutoka mbulu aliyemaliza kwa muda wa 29:30.


Kwa upande wa wanawake Noela Remy alimaliza kwa muda wa 22:14:32 akifuatiwa na Neema Paulo muda wa 22:58:19 wote kutoka klabu ya Talent .
Denisi Malle afisa habari kutoka kamati ya mbio za nyika Arusha alisema katika mbio hizo kwa mara ya kwanza wameweka mbio za watoto ili kuongeza hamasa na ushindani na kuibua vipaji kuanzia ngazi ya chini.
"Ushindani unaongezeka licha kuwa bado hamasa kwa wanawake inahitajika ili ushiriki wao uweze kuongezeka katika mbio zijazo," alisema.
Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabuday aliwapongeza waandaaji kwa kuendelea kusimamia mbio hizo pia kushirikiana mbio za watoto kwa Mara ya kwanza kwani ni jambo ambalo likiwa endelevu litasaidia kuinua vipaji vya vijana wadogo.
"Bado nasisitiza kwa mikoa mingine nayo ijaribu kuoga utaratibu huu wa Arusha katika kusaka wanariadha bora watakaounda timu ya mkoa kwa ajili ya mashindano ya taifa,na napongeza Uongozi wa Riadha mkoa kwa juhudi katika kusaka wadhamini ambao ni Posso International 'USA' na Sunrise Radio kwa kuwaunga mkono," alisema Gidabuday.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya mbio za nyika Rogart John Stephen aliwasihi wanariadha wote wajiuokeze kushiriki kwani ndio yatakayowaweka katika nafasi bora kwani wataendelea kuhamaisisha mchezo huu na jamii iruhusu watoto wao kushiriki Riadha.
"Tunashukuru wadhamini wote wanaojitokeza katika kuisaidia maendeleo ya mchezo huu na tunawaomba na wengine wajitokeze kuisaidia mchezo huu upige hatua zaidi," alisema Rogart


Hivyo makala Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika

yaani makala yote Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/riadha-nyika-wanariadha-wachuana-vikali.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Riadha /Nyika : Wanariadha wachuana vikali mbio za Nyika"

Post a Comment